KAMPUNI ya Mnafu Enterprises imeahidi kutoa zawadi ya seti moja kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa FC) kwa ajili ya matumizi katika michezo yake mbali mbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mnafu Enterprises, Mnafu Mmary alitoa ahadi hiyo juzi mara baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu Taswa FC na Salasala Vision Group (SVG) Veterans iliyofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club.

Mmary ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa timu hiyo ya Salasala alisema kuwa amevutiwa na timu hiyo ya Taswa FC kwani wamedhihirisha kuwa wanaandika kitu ambacho wanakijua.

“Nimefurahi jinsi mlivyocheza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, nimehamasika sana kwa mchezo wenu na ninaamini kuwa mtaendelea kufanya vyema,” alisema Mmary.

Alisema kuwa atakabidhi jezi hizo kabla ya mechi yao ya marudiano iliyopangwa kufanyika Juni 22 kwenye uwanja wao wa Salasala. Katika mchezo huo wa kuanzisha ushirikiano, Taswa FC iliibuka kwa mabao 3-2 yaliyofungwa na Majuto “Ronaldo” Omary alyefungwa mawili yote kwa njia ya mipira ya faulo ndogo nje ya eneo la hatari na Dennis Bukoli kwa njia ya penati.

Mabao ya SVG yalifungwa na Paul Muache kufuatia pasi safi ya Peter Marwa na Yahya Mbanka baada ya kazi nzuri ya Charles Mtangi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2013

    jamani hivi hao wachezaji taswa mnawapima afya zao?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...