Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Juma Kaseja akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Pullman ilikoyo Marrakech,nchini Morocco.Kushoto ni Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen.
Marrkech, Morocco
Huku Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi) dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia, Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.
Kocha huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.
“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.
Alisema suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars, inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Alisema Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika mechi hii,” alisema.
Poulsena alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.
“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
Naye nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya kuelekea Marrakech.
“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara nyingine kwa kushinda mechi hiyo.
“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.
Stars iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na Gambia 1.
Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania.
Baada ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu.
Zetu dua kwa Taifa stars!
ReplyDeleteWadau, naomba mnisaidie kama mna link ya tovuti mnayotumia kufutatilia michezo ya mpira wa miguu; specifically mechi hiyo ya Morocco baina ya nchi yetu.
ReplyDeleteNaomba ku-confess, mimi si mshabiki wa mchezo huu ila huwa nafuatilia kila miaka minne wakati wa Kombe la dunia.. na hii ni mara ya kwanza natarajia kuangilia kwa hamu mchezo huu wa 'World Cup Qualifier'.
All the best Taifa Stars!
Homesick Tanzanian..
Ali..
GMT +1
Mdau jaribu mtandaoni kwa link hii p2p4u itakuonesha mechi zote za leo then utachagua
ReplyDeleteYap! Nimepitia hio link sasaivi mechi TZ vs Morocco saa tatu usiku live. mdau ukerewe
ReplyDeleteWadau saidieni ombi la mwenzetu kwa anayejua hatamie natamani kushuhudia hilo game! Mungu ibariki stars ishinde na iendelee kushinda ili nasi kwa mara ya kwanza tuwakilishwe Brazili kwenye World cup 2014.
ReplyDeletehttp://www.firstrow1.eu/ ama http://www.viplivesports.eu/sports/football.html
ReplyDeleteboli linaanza saa ngapi kwa saa za huku ughaibuni? wadau tujuzane tupate kujionea timu yetu ya taifa stars ikiwapiga bao 2 wamorroco huko nyumbani kwao marakech
ReplyDelete