Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...