Instabul,Uturuki: Baada ya maandamano ya wiki tatu katika mji mkuu wa Istanbul,nchini Uturuki,
Mapema leo wandamanaji waliamrishwa kuondoka mara moja katika viwanja vya Taksim Square,Istanbul,amri hiyo ilitolewa na meya wa mji huo Bw. Huseyin Avni Mutlu.
Meya huyo aliwataka wandamaji waondoke katika viwanja hivyo ili
usafi uweze kufanyika wa kusafisha eneo hilo,lakini wandamanaji waliendeleza libeneke la maandamano,Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw.Tayyip Erdogan amekubali kuonana na viongozi wa maandamano hayo
siku ya jumatano na kusikiliza matakwa yao,lakini kabla ya viongozi hao
kuonana na waziri mkuu wa nchi hiyo.
Askari wa kutuliza ghasia (kina Ras makunja) wa nchi hiyo wameshavamia viwanja vya Taksim Square na kuwarushia wandamanaji milipuko ya machozi,maji ya kuwasha na mkong'oto kama ilivyo mila na desturi yao
kina ras makunja(FFU).
kwa undani ya habari hii, bofya hapo http://www.abc.net.au/news/2013-06-11/police-take-taksim-square/4747650
kina ras makunja wa uturuki wakipereka na muziki wao hewani
MAMBO YA UTURUKI HAYATUHUSU.
ReplyDeleteMambo Uturuki yanatuhusu dunia imekuwa kijiji,watanzania kuna vitu vingi vya kujifunza,kenya walipopata matatizo tulisema hayatuhusu...baadaye nasi yalituka
ReplyDelete