Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki.
Asklari kanzu akiwa na bastola alikamatwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.
Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
Neno kwenye Pikipiki waliyokuwa wakitumia hao.
Ofisa wa Polisi akijaribu bastola waliyokutwa nayo watu wawiliwaliokuwa katika Pikipiki Posta Mpya jirani na Benki ya Posta leo.
Heee ina risasi!
Mtu aliyekutwa na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa na kuchukuliwa maelezo.
Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabili gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji mtuhumiwa.
Nimependa hilo neno kwenye pikipiki
ReplyDeleteWalijuaje km anabastola km c mwajuana sasa mwaanza kugeukana kwenye saliyo
ReplyDeleteSasa hawa mapolisi kanzu mkianza kuwaanika hapa si waarifu watawatambua bwana. Funika uso kidogo na photoshop.
ReplyDeletehaha wamekamatwa na bastola lakini wamekaa kama marafiki na hao polisi hata wasiwasi hawana na polisi wanawapa ruhusa ya kuwasiliana na simu kama kawaida kweli bongo muozo
ReplyDeletehuku ughaibuni ukikamatwa kwa kosa lolote au kushukiwa na jambo lolote kitu cha kwanza wanakusachi mifukoni wanachukua kila kitu chako na ukifikishwa kituo cha polisi hupewi nafasi ya mawasiliano ya simu mpaka baada ya siku 3 kwa maana hiyo muda huo wote watakapokuwa kwenye uchunguzi hutoweza kuwasiliana ili kuharibu uchunguzi wao
sasa hapo bongo watuhumiwa wanaruhusiwa kuongea na simu ili wajipange na watu wao kujenga majibu kwenye maswali watakayoulizwa ili ionekane walikuwa hawana nia mbaya.
bongo badobado sana labda mpaka 2050.
kidhibiti kinashikwashikwa tu ovyo namna hiyo kweli
ReplyDeletekidhibiti kinashikwashjikwa tu ovyo namna hiyo duh
ReplyDeleteHiyo nimewipenda tena muwakague vizuri humo kwenye mifuko wanamabomu pia, halafu muulizeni pia yule mwenzake alielipua Bomu kule Arusha yuko wapi? na aeleze vizuri.
ReplyDeleteWee unakaa ughaibuni ipi ambyo mtu akikamatwa haruhusiwi kuwasiliana na wenzake.
ReplyDeleteWacheni kudanganya watu na ughaibuni yenu.Hayo wameanza leo!
N polisi wakikamata haya wanaanza kuumbuana na watu wanaojuana nao,wasipokamata polisi wa bongo hawajui kazi.watu mnasikitisha sana hata hamwleweki mnataka mvua au mnataka jua.
Hizo zinauzwa kama njugu sasa kila mtu anayo, akifika police atatoa risiti aliyonunulia basi, sheria ina mruhusu kutembea nayo
ReplyDeleteMdau uko ughaibuni gani? Ambako mtuhumiwa hana haki hata ya kuwasiliana na wakili wake? Na hivi mnajudge vipi kosa kwa picha? Kwani kuwa na bastola ni kosa? Hebu vyombo vya habari kuweni na weledi, fanyeni uchunguzi, muwahoji polisi maswali ya msingi na muandike kitu cha kueleweka!
ReplyDeleteKAMA SIO MCHEZO WA KUIGIZA BASI HONGERENI SANA POLISI. LAKINI HAO WOTE WANATAKIWA WASHUSHWE VYEO KWASABABU KUANZIA LEO SIO ASKARI KANZU..WAMEKUA ASKARI WAAAZI. HATA MIMI NA WEZI WOTE WAMEAWATAMBUA. PILI WALIBEBA WAANDISHI WA HABARI KUCHUKUA TUKIO? WALIJUAJE HAKUTATOKEA MAPIGANO? LAKINI KAMA MWINGINE ALIVYOSEMA UTAMPAJE MUDA AWASILIANE NA SIMU???? HIYO SIMU INATAKIWA IWE SEHEMU YA UCHUNGUZI. UKITILIA MAANANI KUWA KUNA MATUKIO MENGI YA WIZI WA SILAHA KWA KUTUMIA PIKIPIKI?? HATA HAWA ASKARI WACHUKUIWE HATUA.
ReplyDeleteBado hatujafika.Askari anashika bila gloves sasa hizo finger prints ?Cha ajabu zaidi badala ya kwenda kituoni kuwauliza kupata habari kamili wao kila kitu hapo mtaani .Jamani sihata wawe wanaangalia mves zenye juh kazi zao wajifunze
ReplyDeleteHawa jamaa wanaonekana si majambazi hiyo Bastola ni ya kujilinda wao wenyewe .. Jambazi ukiliona tu unalijua.. Watu wenyewe hata wasiwasi hawana bana. Labda am so naive to judge people according to their looks but the body language tells the all story, am convinced these people are legally gun holders.
ReplyDeletehee sasa wakikana mahakamani kama sio yao wapepandikiziwa tu na polisi tizama fingerprint polisi si watakuwa wamekwisha mmhhhh bongo kunaendeshwa ki kariakoo kariakoo tu.
ReplyDeleteAnony wa nne toka juu umesema kweli. Kumpa mtu ruksa ya kuongea na simu mara baada ya kutuhumiwa sio jambo la maana. Ukitembea na siraha lazima uwe na kibari chake. Askari kanzu munaweza kusitukia munavamiwa! Harafu hapo hapo hawa watuhumiwa wangepigwa pingu chapu chapu. Kweli Bongo......
ReplyDeletewapi mnafahamiana nyie,sema upande wa salio ndo zengwe hapo!
ReplyDeleteKwani mtu haruhusiwi kuwa na bastola kama ameichukua kihalali? Tusitoe majibu kabla ya polisi kwani yawezekana wanamiliki kihalali. Tusibiri majibu ya polisi ndipo tutoe tuhuma, sio mnakurupuka tu.
ReplyDeleteYANI HAWA WANAOPAKIZANA WATATU KWENYE PIKIPIKI MARA NYINGI NI WAARIFU HII NIMESHUHUDIA JUZI,NILIKUWA NIMEPITA MITAA YA MIKOCHENI NILIKUWA KWENYE USAFIRI BINAFSI,GAFLA NIKASIKIA KISHINDO KIKUBWA SAANA KUMBE WALE JAMAA KUNA KIJANA ALIKUWA NA BODABODA HUWA ANATOKA KWENYE BIASHARA FLAN WAMEMSOMA,JAMAA ALIVYOVYATUA YA KWANZA ANATAKA KUFYATUA YA PILI,ILE BASTOLA IKAANGUKA CHINI WA BAJAJI AKAIOKOTA IKABIDI WA PIKIPIKI WAKIMBIE
ReplyDeleteKwani mtu huruhusiwi kutembea na bastola yako unayomiki kihalali? mbona watu kibao sana wanazo mjini na wanajulikana, mbona hawakamatwi, au ndo mlijua kuwa hao jamaa wanataka kufanya uhalifu? sijaelewa!
ReplyDeleteSiku hizi Tanzania huwezi hata kwenda bank maana ukitoka hata na million moja unapigwa risasi una tolewa uhai wako!!!! Watu wa Bank wana wasiliana na watu wabaya/majangili halafu unanyang'anywa pesa na kuuliwa na watu waendeshao piki piki. Haya wawataje na wenzao sasa.
ReplyDelete
ReplyDeleteJeshi la polisi linaumuhimu wa kurejesha maofisa wake kwenye mafunzo au wapatiwe refresher courses mara kwa mara ..KIZIBITI UNAKISHIKAJE NA MIKONO YAKO BILA GLOVES ....SASA FINGER PRINTS SI ZITAKUWA ZA ASKARI mmhhhhhh
Wasi wasi wangu ni pale mtuhumiwa atakapoikana hiyo Bastola na Askari kanzu keshaipapasa bila hata gloves.
ReplyDeleteKaazi kweli kweli. Hiki kituko jamaa kapanda kwenye Boda boda kasimamishwa kakutwa na bastola. Polisi bila kuchunguza kama anaimiliki kihalali au laa! wanamdhalilisha kwa kupiga picha na kuweka kwenye vyombo vya habari. Ikibainika kama anamiliki kihalali jeshi la polisi litamuomba radhi? na kupanda pikipiki na kuwa na Bastola ni kosa siku hizi? Kwa kuwa majambazi wengi wanatumia bodaboda basi wote wanaopanda usafiri huo na kuwa na Bastola ni wahalifu?
ReplyDeleteKwa kweli inanistaajabisha na jamaa akiwa ana miliki kihalali hawaoni watakuwa wamesha hatarisha usalama wake kwa kuweka wazi aina ya silaha anayomiliki?
Jeshi letu la POLISI halifundishwi privacy? siyo kila jambo ni la kuweka hadharani wakati mwingine wanahatarisha usalama wa wananchi. Wana USALAMA wetu wasipende "CHEAP POPULARITY AT THE EXPENSE OF DAMN INNOCENT CITIZEN" siungi mkono UHALIFU NA WAHALIFU bali napenda Polisi izingatie privacy ya raia wema wanakimbilia piga picha akiwa ana miliki kihalali je? Wanataka vyeo kwa kuonekana wanafanya kazi?
Kingine inakuwaje KIZIBITI kinashikwa hivyo na polisi tena pasipo hata kuwa na gloves akimruka kuwa ni yake atafanyeje maana kama imetoka kwenye kufanya UHALIFU hicho kitakuwa kimbembe chake anashikaje kizibiti bila hata protective gear jamani? Hawa polisi wetu wanafundishwa kweli? angalia alivyoshika kama MAANDAZI hahahahah!
Usanii mtupu. Hapo police wamepata mlo wa leo. Rafiki yangu ana supermarket, pia ana camera dukani. Alipoibiwa kawashika wezi na ushahidi ni ule mkanda. Kawapeleka kawe police. Walilala siku 2 tu, walipopata fedha ya kuwapa police wakatolewa na mkanda ukapotea. Chezea police ya bongo wewe!
ReplyDeleteNapenda sana namna polisi wanavyoendesha shuhuli zao nchini. Askari anapakatia ushahidi namna ile peku peku hakuna haja ya kuhifadhi alama za vidole kwenye bastola hizo kwa sababu watakalo sema kortini hakimu atawaamini. watuhumiwa wako free na hata hawana wasi wasi na wanacheka ingawa wanatuhumiwa kukutwa na silaha hatari sana. Na mwisho ingwawa watuhumiwa wamekutwa na chombo chenye kuweza kusababisha kifo hakuna kurusha rungu lakini subiri kwenye mkusanyiko wa watu huko ni rungu ni rukhsa.
ReplyDeleteTanzania tambarareeeeeeeeeeeee
Anony hapo juu muongo sana, Ukikamatwa Ulaya unapewa haki ya kupiga simu 3 kila baada ya muda fulani. kati ya hizo simu 3 ni ya wakili na kama hauna wakili unatafutiwa. Na kama hauna wakili una haki ya kutokubari kuojiwa bila ya kuwa na wakili ktk hayo maojiano.
ReplyDeleteGood job askari wetu, angalau tuwape sifa. Lakini hicho kidhibiti kinashikwa na na polisi bila gloves wala nini, yaani bare hands like that? Sasa finger prints zinakuwa za kwao tayari ushahidi umeshapotea.. Askari wetu inabidi wafuate professionalism katika kukamata watuhumiwa na vidhibiti na kuhakikisha hawaharibu ushahidi baada ya kufanya kazi kubwa yote hiyo..Japo is too early to judge, kama ni kweli hali hii inaogopesha kwani hawa Watuhumiwa huwezi kudhania kuwa wanaweza kuwa majambazi au kubeba bastola..
ReplyDeleteJe anaimiliki kihalali????????????
ReplyDeleteHalafu na wewe mdau wa Ughaibuni??? ni ughaibu gani huo wa kumuweka mtu siku tatu bila mawasiliano? au Manzese hiyo?
Hakuna ughaibuni ambako mtuhumiwa harusiwi kuwasiliana na jamaa zake au wakili.Hapo mdau umechemsha na umedanganya.Omba msamaha kwa wadau kwani haya mambo ya ughaibuni ulikuwa huyajui vema.
ReplyDeleteMnadhani gloves ndo zinasaidia sana hadi mkalaumu watu kushika bunduki bila gloves!Kinachojaliwa sana ni record ya bunduki,je mmiliki ni yeye?Yaani aliyeshikwa nayo ndiye mmiliki.Kama siye gloves za nini.Gloves zinatumika sana kama bunduki imekutwa kwenye tukio au la mapigano ama mauaji lakini haiku mikononi mwa mtu.
Lakini pia cha msingi ni kile alichosema mdau kuwa ngoja kwanza tuwasikilize polisi na uchunguzi wao.Tusihukumu tu.Maana mahakimu wa mitaani tuko wengi.Kukutwa tu na bunduki si neon,labda ndiye mmiliki,au naye yupo kazini ila tu hawa waliomkamata hawajuani naye bado.
Nakumbuka kisa kilitokea siku moja tulikuwa kwenye basi la Buguruni Posta,abiria mmoja alikuwa na pisto kiunoni,ilionekana na abiria mwingine kwa kuwa mmiliki alikuwa ameshikilia bomba hivyo shati lake limeinuka juu.Abiria wakabonyezana hadi kumweleza dereza ambaye naye akachepuka na gari kuingia kituo cha polisi.Konda ghafla akawaita polisi ndani ya basi kuna mtu anabunduki pisto.Mara yule jamaa akakamatwa kutiwa kituoni.Katoa kitambulisho kumbe ni afisa wa usalama jeshini alikuwa kazini.
Yaani huyo askari kwenye picha ya kwanza kabisa ndio kafurahisha jamii!! unakamata bastola na index finger kwenye trigger on a loaded gun??? usalama uko wapi hapo??? du kweli umechemsha!
ReplyDelete