SIKU moja baada ya Simba kumalizana na mchezaji wake Amri
Kiemba (pichani), mchezaji huyo sasa yupo sokoni na atauzwa kwenye timu ya
Wydad Casablanca ya Morocco.
Kiemba alimwaga wino wa kuichezea Simba kwa miaka miwili jana
kwa dau la Sh35 milioni huku atakuwa akikunja mfukoni kitita cha
Sh2 milioni kama mshara wake.
Awali mchezaji huyo alikuwa akiwaniwa na mahasimu wao Yanga, na
Simba ingezubaa basi kiungo huyo angerejea nyumbani kwa
mabingwa hao wa Tanzania bara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Zakaria Hanspope tayari
ametua Morocco akitokea Tunisia ambako alikwenda kufatilia fedha
zao za usajili wa mshambuliaji wao Emanuel Okwi anayekipiga
kweney timu ya Etoile du Sahel nchini Tunisia.
Okwi alijiunga na timu hiyo ya Tunisia mapema mwaka huu baada ya
Simba kumuuza kwa dola 300,000 lakini klabu hiyo ya Etoile Du
Sahel imekuwa ikizingua kulipa fedha hizo.
Lakini jana Hanspope alisema "Nimeshatoka Tunisia nipo Moroco na
nimeshafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Wydad
Casablanca n kesho tunafanya mazungumzo ya mwisho kabla
sijarejea Dar, kila kitu kinaenda vizuri, naamini tutafikia mwisho
mzuri."
Simba waliingia mchecheto wa kumsajili mchezaji huyo baada ya
kutonywa na kigogo mmoja wa TFF ambaye pia ni mnazi mkubwa
wa Simba kuhusu timu hiyo kuvutiwa na Kiemba na kushauri
asajiliwe haraka ili Simba wapate faida kwa kumuuza.
Casablanca walimuona mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya
Stars na Morocco ambapo Stars ililala kwa mabao 2-1 goli ambalo la
ni kufutia machozi lilifungwa na Kiemba.
Ukisikia mpira wa Bongo unakwenda ki Simba na Yanga ndio hivyo. TFF hakuna professinalism yeyote na hapo ni hakika atakula commission kwani alijuwa kuna ulaji ndio akawaambia Simba wamsajili haraka lakini si kwa manufaa ya mpira wa Tanzania. Ulafiii.
ReplyDeleteAnonymous maneno yako kisu maana sina hata la kuongeza bali kusema swadakta bro....
ReplyDelete