Siku moja baada ya Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuziteua timu za URA, Elite Sport ya Chard na Rayon Sports ya Rwanda kuziba nafasi za timu za Tanzania, Serikali jana imetangaza kuziruhusu timu hizo kushiriki michuano hiyo iliyopangwa kuanza Jumanne ijayo Juni 18 Durfur nchini Sudan.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amosi Makalla aliiambia jana kuwa serikali ya Sudan imewahakikishia kwa maandishi kuzipa usalama timu za Tanzania zitakazoenda kushiriki michuano hiyo ambayo Yanga ni bingwa mtetezi.

"Tulikuwa tunakataa kwa vile hatukupata taarifa rasmi ya maandishi kutoka serikali ya Sudan kutuhakikishia usalama wa watu wetu kuanzia uwanja wa ndege zitakapotua, zitakapokuwa Khatoum, ulinzi wa kuzitoa Khatorm hadi Durfur na hoteli watakazofikia, lakini jana imetuhakikishia usalama na siku zote Chama cha Soka cha Sudan ndio kilichokuwa kikituambia kuna usalama tusingeweza kuamini, lakini kwa vile tumepata udhibitisho wa serikali timu ruksa kwenda."alisisitiza "Timu zote zilikuwa zinajiandaa na mashindano ni tarehe 18 kama zinataka kwenda ziende, na hao Cecafa kama wameteua timu nyingine iyo ni juu yao."

Makala ambaye juzi alitoa msimamo wa serikali akipigilia nyundo kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe alisema serikali ndio inajua hali ya usalama ya Durfur ilivyo hivyo haiwezi kuziruhusu timu za Simba, Yanga na Super Falcon ya Zanzibar zikashiriki michuan hiyo.

Hata hivyo viongozi wa Simba na Yanga jana walipoulizwa kuhusiana na suala hilo walionekana kuduwazwa kwani hawakuwa na taarifa yoyote ya serikali au TFF ikiwajulisha juu ya jambo hilo, huku timu zote zilishatoa msimamo wa kutoshiriki michuano hiyo baada ya kuambiwa Durfur si salama.

Laurance Mwalusako Katibu mkuu wa Yanga "Ili suala kuna mgongano wa mambo mengi, mpaka sasa hivi klabu hatuna taarifa zozote, na isitoshe sisi jana tumevunja kambi na tumewapa wachezaji wetu mapumziko ya wiki mbili, hata hivyo tukipata tutakaa na kujadili kama tushiriki au la."

Ismail Aden Rage Mwenyekiti Simba "Mi sina habari zozote nipo na Waziri huku (Dom)mbona hajaniambia chochote, ngoja akishaniambia ndio tunaweza kutoa msimamo wetu lakini kwa sasa hatuna taarifa zozote."

Hata hivyo licha ya serikali kuziruhusu hadi jana mchana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa katibu wake Angetile Osiah alisema bado hawajapata taarifa rasmi zaidi ya taarifa ya juzi ambayo serikali waliituma kwa katibu wa Cecafa Nicholaus Musonye ya kutaka wadhibitishiwe kama kweli kuna usalama.

"Rais Tenga juzi aliwatumia barua ya Waziri wa Michezo wa Durfur ya kuwahakikisha usalama wa kutosha kwa timu zetu, zaidi ya hiyo hatujapata taarifa nyingine mpaka sasa hivi." alisema Osiah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2013

    Kwa kuwa tulikwishaamua kutoshiriki ni bora kuendelea na msimamo huo vinginevyo inabidi timu zifanye kazi ya ziada kurudisha morali ktk michezo hiyo. Pili, timu yetu ya taifa inacheza jumapili na wachezaji wengi ni wa timu hizi kwa hiyo hawawezi kupata muda wa kujiandaa na wenzao!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2013

    Kwa nini wanalazimisha!! licha ya kwamba wamehakikishiwa usalama lakini tumeambiwa Darfur hata hoteli hakuna, je watakaa shuleni? Pia ukimuuliza Musonyi suala la usalama Darfur ye atakuhakikishia kuwa upo kwa sababu ye ni muandaaji mkuu. Hakuna haja ya kwenda huko.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2013

    Binadamu unapofanya uamuzi ambao kwanza unasita hapo ni kama unacheza ramli na maisha yako. Kesho husije ukasema, "Oh, kama ningejua.."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...