Bondia Thomas Mashali (kulia) akitia saini ya dole gumba kwenye mkataba wa kupambana kwa ajili ya kuchangia elimu siku ya Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7, mwaka huu katika uwanja mpya wa Taifa jijini Dar. Mashali atacheza na Bondia Patrick Amote kutoka Kenya. Tamasha hilo litawashilikisha wasanii mbalimbali pamoja na wabunge. Kushoto ni Rais wa TPBO, Yasin Abdallah.
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akisaini mkataba kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya katika Tamasha la Usiku wa Matumaini. Kushoto ni Rais wa TPBO, Yasin Abdallah.
Thomas Mashali akipokea sehemu ya fedha za maandalizi kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Patrick Amote katika Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akipokea sehemu ya fedha za maandalizi kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    Huyu hajuia kusoma wala kuandika? ndiyo maana wanadhulumiwa hawa, si ajifunze tu apate tuition.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    Hivi kuna watu bado wanasaini na dole gumba unbelievable hasa ukiangalia umri wa huyo jamaa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2013

    Nadhani kwa suala hili la ngumi utiaji saini kwa dole ni moja kati ya taratibu zao hasa TZ, maana nimeshuhudia wengi tu wakifanya hivyo kwa huko bongo na ndipo nilipoacha kuamini kua wahusika hawajui kusoma bali ndio utaratibu wao.Kwa wakati huu tulionao hata kama mtu hajenda shule kabisa hatoshindwa kuandika jina lake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...