Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka ROCKSTAR4000,Christine “Seven” Mosha , akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kwenye mkutano wao uliofanyika jijini Dar kuhusiana na Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi” kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar 4000.
Pichani shotoni ni Mpoki akizungumza machache kwenye mkutano huo, kati ni Joti na Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani
kutoka kushoto ni Mpoki, Joti, Bobby, Seven, Seki, Masanja na Maclegan
Mpoki, Kitenge, Maulid, Joti, Seki, Masanja na Maclegan
=========== ====================
KUNDI LA KIPAJI CHA
TELEVISHENI KINACHOONGOZA TANZANIA
ORIJINO KOMEDI WASAINI
MKATABA MNONO WA USIMAMIZI
Kundi la kipaji cha
televisheni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia
television imeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana
na Rockstar 4000. Mkataba huu unakuwa wa kwanza kwa wasanii wa luninga
kupitia kampuni hii ya Nexus
Nexus imenunua haki zote za
usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana
nchini kupitia vichekesho vyake kupitia vituo vya televisheni na matamasha
mbali mbali ambapo mkataba huu utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi hiki
cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba wajulikanao kama; Joti, Maclegan,
Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na David Seki ambacho kimekuwepo hewani
kwa mfululizo wa miaka sita.
Kushirikiana na
Orijino Komedi ni kitu cha muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa
ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana
na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo; alisema
Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani.
“Nimefurahishwa sana kufanya
kazi na watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuiingia mkataba na Kampuni
ya Nexus Agency. Kwa pamoja tumedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya
vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa” alisema Christine “Seven” Mosha ,
Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka ROCKSTAR4000.
Muandaji wa vipindi vya
Orijino Komedi, Sekioni Davis ‘Seki’ amesema wanafuraha kuingia mkataba
wa kazi na kampuni ya Nexus Agency na Rockstar 4000 Africa, mbapo ameahidi
kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja
ya soko.
Kwa kushirikiana na
Rockstar 4000, nexus inatambua na kuthamini vipaji hivyo itahakikisha
inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze
kufikia kiwango cha juu vya ufanisi ndani ya Afrika na kimataifa kwa
ujumla.
Jiunge na kufuatilie
Orijino Komedi kwenye:
Website
www.orijinokomedi.com
YouTube
www.youtube.com/orijinokomedi
Twitter
www.twitter.com/orijinokomedi
Facebook
hawa jamaa ni kwishney hawana tena lolote na nawashauri sasa waje tena kiupya kwani hata watoto hawaangalii tena vipindi vyao
ReplyDeleteMbona vengu na wakuvanga hawapo? Au wamewatupa ili msosi uwe mwingi kwao hawa jamaa? Acha uchoyo. vinginevyo hatuangalii tena.
ReplyDeleteHAPAN, WANATAKIWA TU KUWA WABUNIFU NA PIA KUANGALIA WENZAO NJE WANAFANYA NINI. BE CREATIVE NA KUJIUPGRADE
ReplyDeleteNi kweli kabisa, jaribuni kwenda na wakati. Chekesha at the same time fundisha! Watu sasa wanangalia ile comedy ya Star TV. Ipo juu ile mbaya! Unacheka na unapata somo.
ReplyDeleteKwavile mlishajijengea jina basi ushauri wangu ni huo, fanyeni mageuzi ya khali ya juu na haraka iwezekanavyo ili mlete kitu tofauti. Kama alivyosema mdau aliyetangulia, hakuna mtu anayewangalia kwa sasa.All the best! We love you!