Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na wakazi wa Makongo juu kuhusu uboreshaji wa mji huo kwa huduma muhimu za kimji. Kulia kwa Mhe. Tibaijuka ni Diwani wa Kata hiyo Bw. Deusdedit Mtiro na kushoto kwake ni Katibu wa mradi huo kutoka Wizarani bibi Neema Munuo.
Waziri wa Ardhi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Makongo juu Bw. Joackim Shirima wakati akitoa maoni yake kuhusu uboreshaji wa mji huo.
Wakazi wa Makongo juu wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu uboreshaji wa mji huo. Miongoni mwa wakazi hao ni Waziri wa zamani katika Serikali zilizotangulia awamu ya sasa Bw. Ibrahimu Kaduma (wa pili kutoka kulia mstari wa mbele).
Wakazi wa Makongo juu wakiangalia michoro ya ramani inayoonesha mpango wa kuboresha mji huo wakati wa kikao kati yao na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka. (picha zote na Rehema Isango wa Wizara ya Ardhi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2013

    Hongera Waziri Prof.Tibaijuka,
    Sisi wananchi tunajua unania njema ya kuijenga nchi,lakini kinatuchotusumbua zaidi ni utekelezaji na utendaji kazi wa wizara yako,mfano mpango wwa mji wa Kigamboni,wananchi wanaweka pembeni na wanatajikuta hawana chao katika mradi huo,baadala yake wawekezaji wa kigeni na serikali ndio watakao miliki ardhi.kwa sababu utaratibu wa wizara yako afuate sheria za miliki ardhi,kwa nini? serikali isinge wawezesha wenye mali kumiliki ardhi zao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2013

    Muheshimiwa afikege na kwetu Kivule kwa Walalahai. Waheshimiwa wanajisahau sana na Kinondoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...