Kamera ya Globu ya Jamii,mchana huu imewanasa Punda hawa wakipata msosi (wakila majani) katika moja ya Bustani ndani ya Jiji la Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2013

    Usafiri wa Punda, ama Punda kama Kitendea Kazi (Mode of transportation and work force).

    Hii ibaki kama sehemu ya historia na sehemu ya ridhaa na kama mtu kujifurahisha.

    Haiwezekani nchini Tanzania tukiwa na ziada ya Gas, Uranium ,Coal pia Oil baharini tuwe kama Karne ya 12 badala ya kupita Karne ya 21 kwa kutumia mnyama?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2013

    itabidi niende tanga nikawaona punda toka nizaliwe sijawahi kuwaona punda halafu ndo niko majuu mungu wangu ndo walivyo hivi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2013

    Jamani Tanga, na kwengineko Tanzania, huu utamaduni wa kuwaachia wanyama kijilisha wenyewe mijini tumeotowa wapi? Au ndi tumo kumpromote haki za wanyama baada ya kushindwa kwenye haki za binaadamu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2013

    Sio lazima wawe wameachiwa inawezekana wamekata kamba. Labda tuache utamaduni huo lakini wanyama bado wanatumika sana maana hatujatembea lakini ni kawaida kuwaona askari wapanda faras! Af penginepo wakitunzwa vizuri na kutumiwa kwa safari fupi fupi, na kama wataweza kuchunga jinsi wanavyokwenda haja, inaweza ikawa sababu nyingine ya kutunza mazingira kutoka na uchomaji wa mafuta ya gari na pia kupunguza gharama za mafuta.

    Mimi wananikumbusha kitu kingine, dagaa la punda. Kipindi nilipohamia rasmi Tanga mjini 1989 nikitokea kijijini tulikuwa tunakula sana dagaa lililokuwa likitembezwa na mchuuzi mwenye kutumia punda pale barabara ishirini kigutu!


    sesophy

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2013

    Wengi wa wachangiaji nadhani hawaelewi dhima ya ujumbe huu wa picha ya punda ktk hiyo bustani,nalisema hili hasa baada ya kusoma maoni yao.Hali hii ya kuruhusu wanyama/mifugo sehemu ambazo haziruhusiwi imekuwepo kitambo sana Tanzania na bado haikomi licha ya kuwahi kupitishwa maamuzi ya kukamata na kuitaifisha mifugo hiyo.Nilishawahi kuona video moja ndani ya ufukwe wa coco beach mmasai akipita na ngombe, jamani hii kali kwelikweli hasa nikiangalia huku nje nilipo kwa sasa wenzetu wanavyoburudika fukweni kisha mtu anapitisha ngombe????sijui kama angeeleweka, ila kwetu ni jambo la kawaida na ndio maana hata hao punda hapo hakuna aliyestuka nao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2013

    Mpiga picha punda wako wapi hapo? Mimi naona watu watatu. Mmoja mwanaume kasimama shoto barabarani, wawili wanawake wako bustanini tayari. Kwa mbali sana kuna kiumbe wa nne anaonekana kapanda chombo fulani. Swali Je, huyu ni kiumbe gani? na amepanda chombo gani.
    Hiyo ndiyo TANGA.
    Profesa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2013

    Sasa Profesa Mdau wa 6 hapo juu ndio tuseme nini?

    Wewe unataka kuwatisha watu kuwa Punda hawaonekani hapo?

    Labda kumputer yako ina Kimeta haionyeshi picha sawasawa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2013

    Hata mimi namuunga mkono Profesa, kweli hakuna punda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...