![]() |
Dr. Asha-Rose Migiro |
NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.
Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.
Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.
"Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;
"Mmoja wa Watanzania hawa naomba nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.
Kaoneka alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk. Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na mchanganyiko wa neno la Kiingereza hata moja.
Katika kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.
Walisema, athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.
Kaoneka aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni 'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni 'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati usahihi ni "nafanyakazi benki".
Alifafanua kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki wanafanya kazi pamoja.
IMEYATARISHWA NA BASHIR NKOROMO
Kwa kweli Myonge mjonyengeni lakini haki yake mpe! Ni kweli huyo Mama Kingereza kimemkubali lakini anapoongea Kiswahili utadhani lugha nyingine haifahamu. Anakiongea kwa ufasaha na makini. Ni mfano mkubwa wakuigwa. Huku Marekani alikuwa anatupatia changamoto kali ya lugha yetu wenyewe pale tulipokuwa tukikutana naye. Ni mfano wa kuigwa na kujivunia.
ReplyDeleteTupatieni kila wiki masuala ya kuandika na kuzungumza Kiswahili fasaha kwa wadau katika blogu hii ya jamii.
ReplyDeleteMichuzi wewe ni mmoja wa watu wanaofanya tafsiri za moja kwa moja toka Kiingereza kwenda Kiswahili kwenye blog hii hii. Ukome sasa.
ReplyDelete....tehe tehe tehe!!! nadhani neno "ukome" halijachafua hali ya hewa kwa vile neno kukoma kwa kiswahili fasaha maana yake ni "jambo au kitu kufikia mwisho wake"
ReplyDeletekwahiyo kama nimemwelewa vizuri mchangiaji hapo juu ametaka tabia ya kufanya "direct translation" toka kiingereza kwenda kiswahili ifikie mwisha sasa.
Kile fasaha hakipo, taratibuI chatoweka,
ReplyDeleteKimebaki cha mikato, khasa tunachoandika,
Sheti tasikia joto, kisoma ama sikika,
HADHI NA WAKE MVUTO, "KISWAHILI" KINATOKA.
"Direct translation" kiwahili chake ni "tafsili ya moja kwa moja" Tafadhari usiturudishe kule kule kwa wajinga.
ReplyDeleteHuyu mama pamoja na Dr. Mkangara JK kacheza. Wasomi kwa vitendo. Asanteni wamama.
ReplyDelete