Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya ya Singapore leo Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania leo Juni 6, 2013.ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya ndege.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore leo Juni 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi yao jijini Singapore leo Juni 6, 2013. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    Mama Tibaijuka, unaonaje kigamboni ikajengwa kama Singapore hayo ni mawazo yangu tu! Wawekeze huko jamani tunataka kigamboni-singapore.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    Tatizo hao watendaji wakirudi huku its business as usual wanaanza kukimbizana na vikao, warsha, kongamano mwisho wa mchezo nothing is done on the ground. Sasa mkirudi mkae na stakeholders wote (NHC. NSSF, PPF, TBA etc) mpange mikakati ya pamoja sio huu ushindani wa nani ana gorofa refu zaidi (TPA walirudia kuchora jengo lao ili wawazidi PSPF).

    Che

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    Rudini na jwabu kamili la kwa nini Singapore imejikwamua!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2013

    Anony unaeshauri kigamboni ikajengwa kama singapore, mie nafikiri wazo lako si baya ila liboreshwe kidogo, kigambonikwa sasa kuna investment kubwa ishafanywa na watu binafsi na serikali, hivyo ni gharama kuhamisha hivyo kwa nini tusijenge hiyo "singapore" mafia au "ukerewe" kama ni kufuata maji. lakini kama si lazima kisiwa basi tutafute polri lolote kwa kuwa nchi yetu kubwa ambayo haitahitaji fidia au kama itakuwepo ni ndogo tu, tujenge hiyo singapore, tusiwe na mawazo mgando kila kitu dar, opportunity zote ukiweka sehemu moja ndio inakua vurugu coz kila mtu atataka kuishi hapo. ni mawazo tu.
    Mbegu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2013

    Inasikitisha kila siku tunasafiri maranyingi kwenda kujifunza sio wakubwa tu hata wafanyakazi wa kisekta. Kinachotakiwa ni kuthubutu hakuna kingine. Kuna vitu vingine havihitaji kwenda nje ya nchi kujifunza. Mfano, Kuondoa foleni DSM, Kuzibua mefereji ya maji jijini, kusambaza umeme kwa bei nafuu, kugawa viwanja vilivyopimwa na kupangiliwa. Mwakyembe: Kutoka G.Mboto mpaka Sullender it is a canal (jengeni iweze kusafirisha watu na mizigo), anzisha usafiri wa majini toka Kurasini - na mbweni/Bagamoyo to Posta, tandika reli toka Boko - tegeta mbezi luis mpaka G.Mboto to chamanzi. These are posible. Mapato yapo (Migodi, GESI na kodi za wananchi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...