Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ambaye yuko nchini kuhudhuria Mkutano wa Global Smart Partneship jana alitembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuvutiwa na mandhari nzuri ya Serengeti iliyosheheni wanyama mbalimbali. Rais Rajapaksa aliwasili asubuhi jana na kufanya safari ya utalii wa siku (day trip) akiwa amefuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki. Katika muda mfupi aliotembelea Serengeti aliweza kujionea wanyama mbali mbali kama vile Simba, Tembo, Twiga na makundi makubwa ya pundamilia na nyumbu.

Aidha, kufuatia kuvutiwa na uzuri wa Serengeti Rais Rajapaksa aliahidi kutembelea tena hifadhi hiyo mwezi ujao akiwa na familia yake ili waweze kujionea uzuri wa hifadhi hiyo akiwa na muda wa kutosha pamoja na familia yake.
Rais Mahinda Rajapaksa (katikati) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Anjelina Mabula mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Rais Mahinda Rajapaksa akiaga mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2013

    Hivi viongozi wa nchi nyingine wakija kutembelea nchi yetu kwa mapumziko (vacation) na kutembelea mbuga za wanyama, kuna umuhimu gani wa kupelekwa na viongozi wa kiserikali huko? Hiyo bajeti ya kumgharamia Waziri kufuatana na kiongozi wa nchi nyingine kwenye mbuga za wanyama inatoka wapi kama sio kodi zetu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2013

    watanzania suti na mbuga za majani ni sawa kuweka ndimu kwenye chai ya maziwa,na wakati huo huo ujaribu kuchovya vitumbua ndani ya chai hiyo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2013

    watanzania bado tupo nyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuumaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sana tuuuuuuuuu

    viongozi wanavaa suti kwenye mbuga za wanyama badili ya kuwa mfano kwa kuvaa vazi maalumu kwajili la mbuga za wanyama

    hata huyo mgeni kawashinda na anawashangaa watanzania tumezidi kupita kiasi sutiiiiiiiiiii kila sehemu

    vazi la suti tumelipenda sana watanzania lakini ni ushamba wa hali ya juu ushamba mkubwa sana kujivalisha suti kila sehemu

    aibuuuuuuuuuuuuu aibuuuuuuu tubadilikeeeee!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...