Mtoto
Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar
es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda
mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete
akishuhudia.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa
Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo
asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais
wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais
Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete
alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni
wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo
asubuhi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda
Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo
kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar
es Salaam leo asubuhi.
Rais
Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima
lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda
mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi
nchini.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri
Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa
vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili
leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro).
Hayo matarumbeta yasiwe kati ya vikundi vya kumlaki Rais Obama. Hayana asilia ya ki-Afrika.
ReplyDeleteHivi na kikwete akienda uko mbele analetewa ngoma adi airport ?
ReplyDeleteDuu, kanchi kadogo hivyo wana dege kubwa hivyo, wabongo Gulf stream 55 tu hapakulalika.
ReplyDeleteNimefurahishwa na mavazi yao ya taifa,yule Muswati hadi hirizi nayo ni sehemu ya vazi,huyu naye hadi skafu ni sehemu ya vazi la taifa, hiviii? ule mchakato wa vazi letu la taifa uko hatua gani?
ReplyDelete