Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.

Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.

Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14
Redds Miss Nyamagana 2013/14 Rosemary Peter katika pozz, mara baada ya kutawazwa rasmi kushika taji hilo, katika hafla fupi iliyofanyika katika hotel ya New Mwanza ya kumvua aliyekuwa akishikila taji hilo Mrembo Diana Amimo baada ya kudanganya Urai wake na Umri.
Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Sash Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013.
Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    JAMANI NYAMAGANA IKO TANZANIA AU BURUNDI?NAOMBENI JIBU JAMENI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2013

    iko mwanza

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2013

    Nyamagana ipo TANZANIA ipo BUGUNDI na pia ipo UGANDA.

    Katwe ipo TANZANIA, ipo BURUNDI na pia ipo UGANDA.

    Kariakoo ipo Dar Es Salaam na Lindi TANZANIA ipo pia Mombasa-KENYA.
    ...................................
    CHILIA MBALI MAJINA YA MAENEO , ANGALIA MAJINA YA WATU MFANO CHINI
    ...................................
    KAMUGISHA ama MUGISHA yupo TANZANIA, yupo UGANDA na pia RWANDA.

    ONYANGO yupo TANZANIA, yupo KENYA na pia yupo UGANDA.

    OLE SAIBURU, OLE NAIKO yupo TANZANIA na pia yupo KENYA.

    Hilo SIO TATIZO sio ajabu majina kuwepo miongoni mwa nchi hizi, HUO NDIO UHALISIA ZAIDI WA KUTHIBITISHA UNDUGU KTK ENEO LETU HILI na hii ni AFRIKA YA MASHARIKI!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2013

    Haya ndio matokeo ya ucheleweshaji wa kutolewa kwa wananchi wote Vitambulisho vya Utaifa.

    Tusije Kushangaa Afisa wa Kiseriklai ama Mkuu wa Idara ya Serikali nchini Tanzania akawa Mrundi, Maganda, Mkenya ama Mnywarwanda!

    Mlikuwa wapi hadi 'Banyamulenge' anavikwa Taji la Ulimbwende ktk aridhi ya Tanzania?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2013

    Ohhh Makubwa!

    Mbona Wageni Majirani zetu watatuburuza sana?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2013

    Ndio maana Serikali yetu inachelewesha masuala ya Afrika ya Mashariki!

    Mmeona mfano ktk Mashindano hayo?, Mgeni ameweza kupenya na kunyakua Taji!

    Sasa huo ni uzuri tu, je Fursa za Kiuchumi mbele za Wageni mnafikiri tupo salama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...