Tanzania imenyakua Tuzo tatu za Ubunifu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika. Tuzo hizo zimetolewa wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika jijini Accra.
Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana, jijini Accra ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, akimwakilisha Waziri wa Nchi-Utumishi Mh. Celina O. Kombani (MB), ambaye pia ni Mwenyekiti wa mpito wa Mkutano wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika alisema ni muhimu watumishi wa umma Barani Afrika kujikita katika ubunifu ili kuleta tija, kwa tasisi na wateja wanaowahudumia. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi pamoja watumishi wa umma kutoka sekta mbalimbali Barani Afrika.
Awali, Mkuu wa Watumishi wa Umma nchini Ghana Mh. Prosper Douglas Kweku Bani alisema mchango wa watumishi wa Umma Barani Afrika unatambuliwa lakini mwisho wa siku atakayetia jitihada zaidi katika kazi yake lazima atunzwe ingawa "wote ni bora na lengo ni moja".
Tanzania imenga'arishwa na Taasisi zifuatazo, Wakala wa Vipimo (WMA), Nida na NAO. baadhi ya matukio yaliyojiri katika Ikulu ya Ghana wakati wa hafla hiyo ya utoaji Tuzo za Ubunifu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akisoma hotuba katika Ikulu ya Ghana wakati wa utoaji Tuzo za Ubunifu kwa taasisi za Umma mbalimbali Barani Afrika.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Watumishi nchini Ghana, aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, Mh. Propser Douglas Kweku Bani akitoa hotuba yake kabla ya utoaji Tuzo.
Wawakilishi wa Wakala ya Vipimo (WMA) wakipokea Tuzo toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Watumishi nchini Ghana Mh. Propser Douglas Kweku Bani (kushoto) aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana jijini Accra.
Wawakilishi wa NAO wakipokea Tuzo toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Watumishi nchini Ghana Mh. Propser Douglas Kweku Bani (kushoto) aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana jijini Accra.
Raha ya Ushindi, wawakilishi wa NIDA wakiselebuka na mgeni rasmi Mkuu wa Watumishi nchini Ghana Mh. Propser Douglas Kweku Bani baada ya kukabidhiwa Tuzo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kati kati ya waliobeba Tuzo) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Tanzania baada ya kujinyakulia Tuzo tatu za Ubunifu siku ya Utoaji Tuzo katika Ikulu ya Ghana-Accra.
Kikundi cha ngoma za Utamaduni nchini Ghana kikitumbuiza wakati wa Utoaji Tuzo katika ukumbi wa Ikulu ya Ghana-Accra.
Bendi ya Jeshi la Polisi la Ghana nayo haikua nyuma wakati wa utoaji Tuzo, ilikoleza hafla hiyo.
Kikundi cha kina mama kutoka kusini mwa Ghana kikionesha umahiri kucheza ngoma za utamaduni kwa kutumia vibuyu vikubwa viliyokatwa katikati.
Hongereni sana WMA, NIDA na NAO........ Taasisi tatu kupata ushindi kati ya taasisi 42 za Tanzania zilizowakilisha Tanzania, siyo mchezo! Tafadhali kazeni buti.....
ReplyDelete