Katibu Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali wilayani
Kilwa,Omary Mkuwili akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Mdahalo huo wa
Uwajibikaji wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Chini ya Ufadhili wa The
Foundation na kufanyika jana katika Tarafa ya Pande wilayani Kilwa.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria Mdahalo Huo wakichangia mada
Na Abdulaziz Video,Kilwa
Wananchi wa kata ya Pande, wilayani Kilwa,mkoani Lindi wanakerwa na
tabia ya mbunge wao wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungala Bwege
ya kukwepa kushiriki kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri la muungano
kwa muda Mwingi na hasa bunge la bajeti.
Wakizungumza kwenye mdahalo Unaohusu uwazi na uwajibikaji wa Viongozi
na watendaji wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya wananchi
ulioandaliwa na Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya
Kilwa,(KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for civil socitey na
kufanyika katika shule ya Msingi ya Pande, wananchi hao, Akiwemo Bw
Anan Nahoda, Saidi Athumani Kifuku na Mariamu Kajoka walisema kuwa
muda wote wa kipindi cha mikutano ya bunge huko Dodoma mbunge huyo
uwa hanaonekana mitaani akifanya mikutano ya kuhamamsisha wananchi
wagomee malipo ya pili ya korosho badala ya kuwa bungeni.
Anan Nahoda mkazi wa Pande alisema kuwa,kitendo cha Mbunge wao kukwepa
vikao vya bunge vinawaumiza kwani moja kati ya kazi ya mbunge ni
kuwakilisha mawazo ya wananchi kwenye mikutano ya bunge na kitendo cha
mbunge wao kutokuwepo huko inaonyesha hatimizi wajibu wake ambao
wapiga kura walimchagua hawatekelezewi.
“Kinachotusikitisha sisi tuliomchagua ni kumwona mbunge wetu muda
wote wa bunge yupo nje ya bunge tena kama kuondoka ni leo kwani hata
jana alikuwepo hii inafanya tusiwe na mwakilishi kule bungeni hii si
halali kwani hata akiwepo huku hashughuliki na masuala ya maendeleo
badala yake anaendesha mikutano ya ndani ya kushawishi wananchi
wagomee malipo ya korosho”alisema Anan.
Aidha Anan alilalamikia tabia ya mbunge huyo kutotembelea na
kutofanya mikutano na wananchi ili kukusanya kero na maoni
mbalimbali na kuyasemea akiwa bungeni na kudai kuwa tangu achaguliwa
hajafanya mkutano wowote wa hadhara unaojumuhisha wananchi licha ya
kufanya mikutano ya ndani.
Saidi Athuman alisema kuwa, tatizo la viongozi wengi waliochaguliwa
ni kutofahamu vyema mfumo wa vyama vingi kwani badala ya kushughulikia
matatizo ya wananchi hujikuta wakishughulikia maslahi ya vyama vyao
vilivyowawezesha kuwa madarakani hali ambayo inarudisha nyuma
maendeleo ya nchi na kusababisha uvunjifu wa amani na kuwataka wajue
majukumu yao kwa wananchi waliowachagua.
Kufuatia malalamiko hayo,Mtandao ulimtafuta Mbunge Huyo kwa njia ya
Simu ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo Ambapo Bungala alikanusha
tuhuma za kutofanya mikutano kwenye kijiji na kubainisha kuwa tangu
amechaguliwa amefanya mikutano saba ambapo alikutana na wananchi
mbalimbali kupokea kero zao,na kuhusu la kutohudhuria bunge alikiri
kutokwepa vikao vya bunge na kuwa hivi karibuni alionekana jimboni
kwake na kudai kuwa alikuwa kwenye shughuli za uchaguzi ndogo
ulizofanyika hivi karibuni wilayani Nachingwea ambapo alikwenda ili
kusaidiana na viongozi wenzake kumnadi mgombea wa chama chake(CUF).
“Ni kweli sikuwepo kwani nilikuwa kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo
huku Nachingwea ili kuhakikisha mgombea wetu anashinda na sasa hivi
naelekea bungeni….hoja ya kutoonekana muda mwingi bungeni hiyo si
kweli na ili la kutofanya mikutano si kweli labda huyo aliyelalamika
hakuwepo…. kwani nimefanya mikutano mingi hapo na wa mwisho ni wa
mwezi wa pili mwaka huu”alisema Bungala.
Huyo anayelalamika naona ana maslahi binafsi.Huyu mbunge Bwege anajitahidi sana kuhakikisha wananchi wa kilwa wanapata haki yao. Mfano zao la ufuta, aliacha vikao vya bunge kuhakikisha wananchi wanapata maslahi yao kwenye ufuta. Alichofanya ni kuwaeleza watendaji wa serikali kwamba ununuzi wa ufuta uwe huru kwa kila anayetaka kununua ufuta, lakini bei iwe angalau iwe ile iliyowekwa na serikali, yani kima cha chini.
ReplyDeleteKulikuwa na kubishana sana na wale wanaotaka stakabadhi ghalani, lakini mbunge alihakikisha haki inatendeka kwa wakulima. Matokeo yakawa mazuri, wanunuzi wakanunua ufuta kwa sh 1,600 kwa kilo badala ya sh 1,400 kwa kilo.
Ilulu ndiyo wanataka stakabadhi ghalani, na bei yao waliiweka sh 1,400. Hawakupata hata kilo moja. Na moja ya mfumo wa stakabadhi ghalani ni kwamba unalipwa nusu au kiasi kingine chochote nyingine baadae. Maana yake ni kwamba kama Ilulu ndiye angekuwa ni mnunuzi pekee wakulima wangeuza kwa sh 1,400 kwa kilo, na wasingepewa yote. Wangepewa nusu au kiasi kingine chochote na inayobakia ni siku nyingine. Nadhani kila mmoja amesikia matatizo ya stakabadhi ghalani (Ilulu) katika wilaya ya Liwale, Ruangwa, na Nachingwea.
Kwa hiyo mbunge Bwege anastahiki kwa kuwawezesha wakulima kuuza ufuta kwa sh 1,600 na kulipwa yote kwa pamoja bila mkopo. Ndiyo maana hujasikia malalamiko kutoka kwa wananchi wa kilwa kuhusu zao la ufuta kama ilivyo kwa wenzao wa liwale, nachingwea, na ruangwa.
Wabunge wa namna hii wanahitaji sapoti kubwa toka kwa wananchi ili waendelee kusimamia maslahi ya wananchi kwa maslahi ya nchi.
Muumba ajaalie kheri kwa wananchi na nchi kwa ujumla, na ampatie afya njema na mwisho mwema mbunge Bwege. Aendelee kusimamia maslahi ya wananchi kwa maslahi ya nchi, Muumba amsaidie.
Haya majina yana athari kubwa katika maisha ya binadamu we mwite mtoto Shida kila siktu shida mwite Tabu kila siku tabu haya jina la mbunge Bwege na nyie wananchi bado mnachagua bwege liwaongoze sasa mnalalamika nini si mlimchagua wenyewe.
ReplyDeleteJamani kwani jina linafanya kazi? Kwani mtu kuitwa Bwege ina maana hawezi kufanya kazi? Kuna wangapi wana majina mazuri hawahudhurii bungeni wala kuitisha mikutano kwenye majimbo yao? Tuweni na weledi ktk kutoa mawazo yetu. By mdau
ReplyDelete