Nawasalimu kutoka katika ardhi
jadidu ya mrefu ukaitwa mlima Kilimanjaro, nikipigwa upepo murua unukiao
marashi yakaitwa karafuu, visiwa Unguja nayo Pemba kutengeneza Zanzibar,
alipoishi binadamu akawa wa Kwanza, Ngorongoro kati ya vingi vya kujivunia na
fahari kuitikia.
Labda tumekuwa tukisikia neno
Kioo cha Jamii, na ama baada tukawa tunapeleka fikra zetu moja kwa moja kwa
wale maarufu tunaowaona, kuwasikia ama kuwashabikia, iwe katika Nyanja ya
sanaa, burudani, siasa, biashara, teknolojia na mengineyo kadha wa kadha.
Lakini je tumewahi kuwaza kuwa Kioo cha Jamii ni kila mmoja wetu kwa nafasi yake, iwapo hutajiheshimu na kuiheshimu jamii uliyopo, kuanzia nyumbani, jirani, shuleni, kazini, chuoni, ibadani ama kwingine popote ulipo, wale wakutizamao watawezaje kukua na kuweza kuwa Kioo cha Jamii kile unachotaka wewe kukiona ama ikiwa hata kwako hukuwahi kukitanabahi?
Lakini je tumewahi kuwaza kuwa Kioo cha Jamii ni kila mmoja wetu kwa nafasi yake, iwapo hutajiheshimu na kuiheshimu jamii uliyopo, kuanzia nyumbani, jirani, shuleni, kazini, chuoni, ibadani ama kwingine popote ulipo, wale wakutizamao watawezaje kukua na kuweza kuwa Kioo cha Jamii kile unachotaka wewe kukiona ama ikiwa hata kwako hukuwahi kukitanabahi?
Ujana – Maji Ya Moto
Umeshawahi kuusikia msemo huu,
umewahi kukaa chini na kutafakari maana yake na kisha umuhimu wake? Wale tuwaonao
leo na kuwakebehi, kuwadhihaki na labda kuwacheka kama si kuwadhalilisha kwa
kufikia walipofikia pasipo labda mafanikio ama walichostahili kwa ukubwa leo
umri wao, ushawahi kutambua kuwa nao waliwahi kuwa vijana, damu zikichemka,
mihemko ikihemka na yaliyomo na yasiyomo kujitwisha na kabla hawajatanabahi jua
likazimika na giza kuingia likawafika?
Umaarufu, Jeuri, Makidai na Maisha Yetu
Ushawahi kusikia mtoto akisema
nataka kuwa maarufu akiwa mkubwa? Si kosa wala si vibaya, lakini swali kubwa
unataka kuwa Maarufu kwa sababu gani, ili iweje na kwanini? Ushawahi kusikia
ujumbe wa wimbo ukisema chuo kikuu cha umaarufu bongo ni dharau, jeuri, kiburi
na majigambo? Umewahi kujiuliza kama wewe ni mmojawapo wa wahanga wa chuo hicho
ambacho wakati mwingine ni kigumu mno kuepukika wakati wa ujana na hasa
Umaarufu ama Mafanikio yanapokuja katika umri mdogo?
Maisha YETU, CHAGUO LETU
Maisha ni uchaguzi na labda
huwezi kuchagua uzaliwe katika hali ipi ya kipato, makazi ama ndugu na wazazi,
lakini kwa hakika Hatima zetu tunapokuwa na kuwa na maamuzi yetu, NI UCHAGUZI
WETU. Ushawahi kufikiri ni wangapi wanaoishi kwa maisha ya kuigiza alimradi
waonekane wapo juu, wana fedha nyingi ama mafanikio mengi sana (hata kama
mengine bado ni ndoto wanazoota), wajitutumuao kukidhi starehe, matumizi na
manunuzi yasiyo na chembe ya uwekezaji bali ufujaji, huku bila kujua
wakiendelea kujiongezea msongo wa mawazo, mateso, maisha yasiyo na hata chembe
ya furaha ya kweli na mahangaiko yaliyojaa wingi wa makwazo na maigizo? Kuwa
mmoja kati yao si lazima, ni CHAGUO LAKO, ni MAISHA YAKO.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...