Sehemu ya Meza Kuu (pichani mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina hiyo ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa. .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki akizungumza wakati akifungua semina ya siku ya nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa.Balozi Kagasheki amewaasa Wahariri wa Vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na Serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika Mbuga za Wanyama.
Aidha ameongeza kwa kuwasihi wahariri wa Vyombo vya habari kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu za Majangili ili kutokomeza tatizo hilo sugu la Ujangili.Kagashei alibainisha kuwa yuko tayari kama Wizara kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa Wahariri na Wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa tatizo la ujangili mbugu za Wanyama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ubunge Ardhi,mazingira na Maliasili,Mh James Daudi Lembeli akifafanua jambo kwa msisitizo mapema leo mchana kwenye ufunguzi wa semina ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
Waziri Kivuli (kambi ya Upinzani) Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh Mch.Peter Simon Msingwa akifafanua jambo kwenye ufunguzi wa semina ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa TANAPA,Bwa.Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku ya nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, uliofunguliwa na mgeni rasmi,Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki.Semina hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
Meneja Mahusiano wa TANAPA.Pascal Shelutete akitoa maelekezo mafupi kwa washiriki wa Semina hiyo kabla ya ufunguzi.
Washiriki wa semina hiyo wakiwa tayari ukumbini wakifuatilia yanayojiri.
Pichani juu
ni washiriki mbalimbali wa semina ya siku ya nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga
za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu wajibu wa
Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa,
unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGDPOT.COM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...