Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (wakatikati)akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Zbc Radio Ali Aboud alievaa kanzu kushoto kutokana na kuunguwa kwa Kifaa cha Waya wa Cable na kusababisha Radio kutokusema kwa siku kadhaa kwa kutumia masafa ya Kati (Midium Wave) hapo katika kituo cha kurushia matangazo Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Mhandisi wa Kichina Zhao Wei Min akitoa ufafanuzi wa Kifaa cha Waya wa Cable kilichoungua na kusababisha Radio kutokusema kwa siku kadhaa kwa kutumia masafa ya Kati (Midium Wave)mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alipofanya ziara makusudi ya kuangalia matatizo hapo katika kituo cha kurushia matangazo Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk wakwanza kulia akitoa maelekezo kwa wafanyakazi kuhusu namna ya kutatua tatizo la kuungua kwa Kifaa cha waya wa Cable ambacho kimesababisha Radio kutokusema kwa siku kadhaa kwa kutumia masafa ya Kati (Midium Wave) hapo katika kituo cha kurushia matangazo Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
kwenye ziara ya kikazi waziri hapaswi kuvaa hovyo namna hiyo. hilo shati alilovaa mheshimiwa waziri linapaswa kuchomekewa wakati wote. hata kanzu nayo iwe na maelekezo ni kanzu ya aina gani ili mhusika aonekane amevaa kanzu lakini yuko profesional.
ReplyDeleteWe, acha u-fashenita usiojua!
ReplyDeleteHapo kweli ila, mdau nadhani ungeshangaa zaidi kama tungeoneshwa mguuni kavaa nini?
ReplyDeleteNakuunga mkono, wavae vizuri na waonekane professional, kama "mchina" alivyovaa vile.
ReplyDeleteKweli nilitaka kuandika kuhusu professionalism. Anon wa hapo umeshatoa maelezo ya kutosha.
ReplyDeleteWadau naomba msaada. Katika picha hiyo waziri ni yupi?
ReplyDeleteNdio maana tunataka serikali yetu ili tusiwabughudhi kwa mavazi yetu, kwa akili zako wewe mchangiaji wa kwanza vazi ni bora kuliko ithibati, ari, ukweli na mapenzi ya uongozi?? Hao wanaokufurahisha kwa kuvaa suti ndio hao hao wanaokwiba na kufisha nje huku wengine wakitorosha mchana kweupe.Acha ushamba wewe.
ReplyDeleteUkisema Mhandisi wa Kichina kidogo kama inaleta maana ya Mhandisi feki hivi. Nadhani ingeandikwa Mhandisi kutoka China ingeleta maana nzuri zaidi. #MaoniYangu
ReplyDeleteSijaona ubora wa mavazi ya huyo mchina zaidi ya kutu kwenye macho na mawazo yenu!
ReplyDeleteBesides the mavazi in which I didnot envy the way dressed.What is the solution to the occured problem.Is the kifaa fixed or not.It looks like a lot of porojo going on !!
ReplyDelete