Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikagua gwaride la wahitimu
kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa wa Magereza. Sherehe
hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimvisha cheo cha Mrakibu
Msaidizi wa Magereza, Hamza Abdalla kwa niaba ya wahitimu wa kozi namba 20 ya mwaka
2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa. Sherehe hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa
magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Gwaride la wahitimu kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa
wa magereza likipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani). Dk Nchimbi aliyafunga mafunzo hayo
katika chuo cha maafisa wa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na askari na maafisa
magereza kabla ya kufunga mafunzo ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa wa magereza
kozi namba 20 ya mwaka 2013. Sherehe hiyo ilifanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza
Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...