Home
Unlabelled
Yupi ni Dereva Bora kati ya Hawa??,Angalia kwa Makini Picha hizi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wa kwanza hayuko makini kabisa maana hawezi kuovertake wakati mbele kuna gari lingine linaovertake hata kama alama ya katikati inaruhusu.
ReplyDeleteWa pili naona hana makosa yoyote na yuko makini. Ingawa ni kwenye mlima ila ameamini nguvu ya gari yake na pia alama imemruhusu. Ana nafasi kubwa ya kurekebisha tatizo likitokea.
Wa tatu hayuko makini kabisa kwanza alama haijamruhusu na pia anaovertake magari mengi wakati mbele yapo yanakuja tena taa imeshawashwa kwa tahadhari.
Wa nne ingawa ameruhusiwa kuhama njia lakini hayuko makini.
Wa tano hayuko makini na amevunja sheria.
Kwa maoni yangu WA PILI yuko makini!!
Swali lingekuwa ni yupi mwenye makosa zaidi? Kuwa bora ktk picha hizi kunahitaji maelezo ya ziada!
ReplyDeletehakuna hata mmoja! wote madereva wazembe ambao hawafati sharia za barabarani.
ReplyDeletedereva angalau hapa ni huyu wa basi kwenye picha ya pili toka juu maana alama zimemruhusu na mbele anaona yajayo....huyu mwenye premio ndo walewaleeee na mwenye safari line hapo ndo kaaaz kweli kweli....abiria hapo lazima watakuwa wamesimama huku wameshika viti vya mbele yao..
ReplyDeleteTraffic police wemejificha hapo kichakani wakiangalia nini,walitakiwa kulisimamisha Bus linalo overtake mlimani. Hapo Bongo inaelekea madreva wa mabus ndio wavunja sheria za barabarani. kwanini hakuna alama(road signs)zozote hapo zinazozuia madreva kuovertake hapo mlimani?
ReplyDeleteWote sio Makini japo kuna mmoja angalau kidogo lakini mbele kuna mlima nae si makini ni kuomba Mungu tu,
ReplyDeleteDuh Chinjachinja Live.... Wadau homo ndani ya machinjachinja hayo kimyaaaaa! Aibu yetu daima! Na hutaskia hata hao cjui sumatra takoboa polishi ama tanesco watasemaneno hapo Wooote kimyaaaa Balaa!
ReplyDeleteKuanzia Juu huyu mwenye roli yuko sawa ila bus la Sahara hapa hakuna kitu
ReplyDeletePicha ya pili wote wako sawa maana ili isipokuwa busi japo anaweza kuona mbele na mistari inamruhusu alitakiwa kuwa mvumilivu maana ni kilimani.
Ya tatu hapa T447 CFL hayuko sawa maana magari yote yamepangana hana nafasi ya kuovertake na mbele magari mawili yanakuja sijui atakimbilia wapi wakimbana
Picha inayofuata Mtei Express kachemsha kabisaa ingawa kama nilivyikwisha sema haya magari mawili busi na sijui Cruiser walichemsha nafsi ni ndogo kwa gari linalokuja mbele yao
Hii ya mwisho hawa wawili wote mchemsho
wote madereva bora siunaona wazee wa feva wapo pembeni hapo wanashuhudia watu waki overtake kwenye mlima ndio kwanza wametulia hata hawana tabu alimuhimu wamiliki wa mabasi hayo wanapeleka mlo kwa wazee wa feva mambo yote huwa shwaaaariiii
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu,jibu sahihi la swali lako la yupi dereva, wanalo hao waheshimiwa waliopo majanini picha ya pili upande wa kulia, ni vigumu kweli kuwaadabisha madereva watukutu wasiofuata sheria ikiwa wahusika wakuu wenye mamlaka ya kufanya hivyo wakiwa wanaangalia tena mbele yao mtu anavunja sheria.Ni wajibu wa blog hii kuwaonesha hapa na sisi wadau kutoa maoni yetu lakini iwapo waheshimiwa wakishaamua kufumba macho sidhani kama tutafanikiwa.
ReplyDeleteNo road rules, hiyo in Bongoland.
ReplyDeleteDEREVA BORA NI ANAENDESHA BUS
ReplyDeleteAulizae ataka kujua:Police wawili chini ya mti, je huyo wa tatu kapanda mtini kwa ajili gani?see sec. foto.
ReplyDelete