Mteja wa Airtel mkoani arusha bw, Robert Justin akihesabu pesa zake alizojishindia wakati wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuzitoa kupitia njia ya Airtel Money katika ofisi za Airtel mkoani
Arusha.

 Meneja wa airte Mauzo wa kanda ya kaskazini Stephen Akyooo akikabidhi shilingi milioni 1 kwa Bw, Robert Justine wa jijini Arusha fedha alizojishindia katika promosheni  ya Airtel Yatosha inayoendeshwa na
Airtel maalum kwa wateja  wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kwa wiki, siku au mwezi mbapo pia mteja anaweza kujishindia moja kati ya Nyumba 3 za kisasa zilizopo dar es salaam.

Meneja wa airtel kanda ya kaskazini Stephen Akyoo akiwa na washindi wawili wa shilingi milion moja wa shindano la airtel yatosha kutoka  mkoani Arusha bw, Robert Justine and Balistus Mambo. Washindi wote
walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja walizojishindia katika promosheni ya Airtel yatosha na kuzitoa kwa Airtel Money.

=======  =======  =====

Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya  Airtel yatosha.
•         Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya
pili ya promosheni

Jumapili 28 julai 2013, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imetangaa na kuwazawadia washindi 14 wa kila siku wa promosheni ya
Airtel yatosha shinda nyumba  kila mmoja shilingi milioni moja pesa
taslimu kupitia huduma ya Airtel Money.

Washindi hawa wamepatikana kupitia droo ya wiki ya kwanza na ya wiki
ya pili ambapo jumla ya washindi 14 kutoka katika mikoa mbalimbali ya
nchi walipatikana na hatimaye kukabithiwa pesa zao

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa
Kanda Mkoani Arusha  bwana Stephen Akyoo  alisema” leo tunayofuraha
kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi
zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali na
kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia
huduma za Airtel yatosha  na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali.

nae Meneja Uhusiano wa Airtel Akitangaza majina ya washindi hao bwana
Jackson Mmbando alisema "washindi wetu wa wiki ya kwanza na ya pili ni
pamoja na  Hawa Said Mkazi wa Mtwara, John Masawe mkazi wa singida,
Joseph Emmanuel Nchimbi Songea,  Rosemary Michael na John Masanja
kutoka Tabora , Zuhura Sabuni kutoka Lindi, Balistus mambo kutoka
Moshi, Robert Faustine kutoka Arusha ,  Frank Ladislaus na Paulina
Michael kutoka Sengerema Mwanza, Flavian Adamson Malilo kutoka Katavi,
Jacob Muhole kutoka Dodoma,  Singodi Severin kutoka Kagera  na
Ephrasia Thadeo kutoka Ngara.

Ili kushiriki mteja anatakiwa kupiga  kupiga *149*99#  na kununua
kifurushi cha huduma ya Airtel yatosha cha siku, wiki au mwezi na
kuunganishwa mojakwamoja kushiriki kwenye promosheni na kupata nafasi
ya kushinda nyumba au pesa taslimu shilingi milioni moja kila siku.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Robert Justine
moja kati ya washindi anayetokea mkoani Arusha alisema” nimefurahi
sana kuwa mshindi wa promosheni na ntaendelea kutumia huduma ya Airtel
yatosha ili kuendelea kufaidika na huduma hii na kupata nafasi ya
kushinda nyumba. Natoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii na
kuhakikishia   hata wao wananafasi ya kushinda kama mimi nilivyoweza
leo kukabithiwa shilingi milioni moja kwa kutumia tu huduma ya Airtel
yatosha.

Promosheni ya Airtel yatosha bado inaendelea kwa mienzi mitatu hadi
hapo mwishoni mwa mwenzi wa tisa ambapo mbali na zawadi za pesa
taslimu wateja pia wanapata nafasi ya kujishindia nyumba 3 zilizopo
kigamboni jijini Dar es saalam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...