Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vyakula
vya kufuturisha watoto yatima katika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es
salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa
na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
Airtel Public Relations Manager Jackson Mmbando speaking to reporters
(they are not pictured) at the handover ceremony held at Airtel
offices in Morocco Dar es salaam, followed by Airtel's Social
Responsibility Manager Hawa Bayumi.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi akimkabidhi
mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha
katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa kwa vituo vitatu
vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani) vituo
vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha
hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Airtel Morocco
jijini Dar Es Salam .
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi akiwakabidhi
Saida Makope mmoja wa wakilishi wa kituo cha watoto yatima mjini Dar
Es Salaam katika hafla fupi ya makabidhiano ya vyakula vya
kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa kwa
vituo vitatu vya watoto yatima jijini Dar Es Salaam iliyofanyika
katika ofisi za Airtel Morocco jijini Dar Es Salam akifuatiwa na
mwakilishi wa Bakwata ustadhi Ustadh Hassan Malangali .
Wateja Airtel sasa kupata muda wa dua, nukuu za qurani, mawaidha kwa
kutuma neno Ramadhani kwenda 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku.
Kampuni za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake
cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es
Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa
na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia
watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.
Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne
ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa
wanaohitaji upendo hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa
Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari,
maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na
sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika
makao makuu ya Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma
kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii
tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi
cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.
Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia
Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila
kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha
tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar
Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa kwa mwaka huu
Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango
cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.
Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na
Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa
Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya
Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi
153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za
qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila
siku.
Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila ambaye alikuwa
mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa
fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na
kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa
kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe
mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...