Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru

 Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea  katika makaburi ya Mjimwema
 Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya  mjimwema leo

 Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
 Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
---------------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.

SIMANZI ,Vilio,majonzi  vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati  akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani  na kwamba utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.

Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.

Aidha Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola  wakizani kuwa serikali haipo.
 
Kwa upande wake  Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana  na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.

Kwa upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa  familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia  ili waweze kujengewa nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
 
Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu na jamaa.
 
Rodney Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao. 


habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2013

    Mama, Mungu akutie nguvu na matumaini mapya katika maisha haya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2013

    R.I.P too young to go.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2013

    R.I.P Rodney. Too young too soon!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2013

    Tumepoteza mpiganaji hodari sana katika medani ya kivita.Kwani alitumia mafunzo adhimu sana aliyopata ya ukomandoo na akapambana kufa na kupona na maadui wale wa amani na inasemekana alikua anakaribia kuwaangamiza wote...Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Daima pengo lako ni gumu sana kuzibika kwani mafunzo uliyokua nayo ni wachache sana na wenye moyo wa ziada wanafikia kuhitimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...