Basi la abiria mali ya Kampuni ya Safari, lenye Nambari za Usajili T 9957 BZT likiwa limelala ubavu baada ya Dereva wake kushindwa maarifa wakati akikata kona kali, katika Kijiji cha Ngumbalu, Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.Katika ajali hiyo ni Dereva peke yake ndie alieumia na kufanikiwa kukimbizwa Hospitali kwa Matibabu
Askari Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akiangalia namna Basi hilo kilivyoharibika.
Askari Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akiangalia namna Basi hilo kilivyoharibika.
Pole walio umia
ReplyDeleteLakini tutazidi kusikia mikasa ya ajali kama hizi. Kwani sehemu nyingine za hizi barabara ni mitego ya panya.
Ndugu zanguni, hiyo barabara imewekwa lami kutusaidia na adha ya usafiri haswa wakati wa mvua, chonde chonde spidi bila maarifa hazifai, tutageuza barabara kuwa chinja chinja badala ya changamoto ya maendeleo.
ReplyDeleteombi langu kwa watu wa Songea, Namabengo, Namtumbo hadi Tunduru, barabara itakapo kamilika basi tuitumie kwa busara ilete maendeleo na sio majanga kwa raia wasio na hatia!
Hongereni kwa hatua katika maendeleo ya kusini mwa Tanzania, naiona Mtwara corridor inakuja na neema kwa wantanzania!
Mungu ibariki Tanzania!
Mdau,
Mwenge, D'salaam
Poleni sana wote mliopatwa na mkasa huu. Mwandishi basi hili limepinduka, kupiga mwereka ni kama kufanyia mzaha au kejeli ! Div 0
ReplyDeleteinawezekana kuna uzembe,ila ni vizuri barabara ziwe na alama kama vile kona na pia kiasi cha mwendo kasi dereva anachotakiwa kuendesha,barabara nyingi sana ama hazina alama au alama zinatolewa hatua chache kabla ya eneo husika, mfano vibao vya matuta,mwendo kasi, kona au hata matengenezo yanayoendelea mbele.
ReplyDelete