Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.

Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni 202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.

Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika,

Ripoti hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia 47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku.. 
 
“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.


“Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.” 
 
Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.



Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..  
 
Mpango wa kuleta mabadiliko  
 
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::  
 



· Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.   



· Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .  



· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.  



· Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. . 
 
Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2013

    imetulia

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2013

    Sasa leo hii Mashamba ya Ukoo kule Vijijini watu wanawauzi wakwekezaji halafu wao wakipata fedha wananunulia magari na kujenge Majumba Mijini.

    World Bank imesasambua ukweli wa Umasikini wetu ni kushindwa kuitumia ardhi yetu inavyostahili!

    Hivi kweli suluhisho la ugumu wa maisha ni kuuza shamba au ardhi ya Ukoo huko Kijijini?

    Haitoshi umeuza ardhi ama shamba, fedha tena huwekezi kwenye Mipango endelevu umeona kununua mgari na ujenzi wa Majumba ndio tija?

    JIFUNZENI HOW TO DETERMINE ASSET CLASSES:

    ASSETS:
    -Shamba
    -Ardhi
    -Msitu
    -Mashine ya kuchambulia mazao au ya ku-process madini
    -Nyumba ya Kibiashara

    NON ASSETS:
    -Gari
    -Simu kubwa huku mipango hakuna
    -Nguo nyingi za bei ghali bila malengo
    -Ulevi na sifa (Ujiko)
    -Ngono zembe
    -Sherehe nyingi kupita kiasi

    Tazameni Uingereza ule Ukoo wa Kifalme Jeuri ya fedha wanaipata kutokana na umiliki wa ardhi Karne kwa Makarne hadi hii leo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2013

    Halafu tunaambiwa kuwa shamba unaweza kuliweka rehani ukakopa mapesa benki. Benki zenyewe za kigeni. Ni njia mojwapo ya mabenji ya kigeni kujipatia mashamba endapo utashindwa kuwalipa au kufilisika. Na mabenki yatachukua shamba na kumwuzia yeyote!

    Jifunzeni the agro-revolution ya Uingereza jinsi ilivyoondoa peasantry culture; tumeanza hapa na tutabaki walalahoi tusioweza kukimbilia mijini ili tuajiriwe viwandani, kama huko uingereza ya zamani!

    ReplyDelete
  4. Umesema kweli tupu mdau! Shida Wa-Tz wengi wako ktk hulka ya matumbuzi na kuonekana. Wengi hawa kerwi na ustawi wa kizazi kijacho nao ni pamoja na watunga sera wetu, viongozi wetu. Hii laana ya umaskini wa fikra na hulka ya maendeleo endelivu itafikisha taifa pabaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...