Kaka Michuzi habari ya kazi,

naomba nirushie hii kwa jamii.kundi la Bodaboda Kampen ambalo linajihusisha ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madeleva wa bodaboda wakishirikiana na jeshi la polisi ambapo mwaka huu wamejitolea kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa waliopata ajali za pikipiki,ambapo tulianzia na hospitali ya Taifa Muhimbili na tunatarajia kufanya kila mkoa.

kwa hiyo tunaomba wadau wajitokeze kutupa sapoti katika kutoa elimu kwa waendesha Boda Boda na kuwatembelea mahospitalini pindi wapatapo matatizo kwani mahospitalini wamesahaulika sana wengi wao ndugu zao wapo mbali,kwahiyo wanatakiwa kupata misaada midogomidogo kama nguo, sabuni, mafuta, maji, miswaki, juice, matunda, hiyo ndio misaada tuliotoa jana tarehe 07/07/2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa (Moi).

tunaomba wadau wajitokeze kutusapoti tuweze kutembelea katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam baada ya hapo mikoani na vijijini.

tunatumai ombi letu litakubaliwa kwa wadau mbalimbali.
 Msafara ukielekea Muhimbili.
 Tulipokelewa na Uongozi na kutoa tulichofika nacho.
 Mmoja wa wahanga wa Boda Boda akizungumza na wanahabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2013

    Usafiri wa bodaboda mijini upigwe marufuku kabisa.

    Ila vijijini ni sawa kwa vile hakuna mashindano ya kibiashara na kusababishwa waendesha bodaboda kujihusisha na uhalifu au kuvunja sharia za barabarani.

    Mdau
    Mtoto-wa-Mujini-Orijino

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2013

    Yaani ndio mnazisha kuwapa vichwa hao waeendesha bodaboda waeendelee kuendesha hovyo na miguuizidi kuvunjika, mngeanzisha darasa la kuwasaidia kujifunza usalama Wa barabarani na usalama Wa mnazisha yao kwanza ingekuwa la maana, lakini mnachokifanya sasa ni upumbavu kabisa, kwanini kuwatembelea madereva Wa bodabboda tu, kwanini isiwe kuwatembelea watoto yatima au wagonjwa Wa Kansa? Wajinga Kabisa nyie.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2013

    Mdau wa kwanza kabisaa nakubaliana na wewe mia ya mia, usafiri wa boda boda upigwe marufuku mijini kooote kwasababu boda boda zimekuwa zikiongoza kwa majanga mengi ya uhalifu mijini. WAENDESHA BODA BODA WAMEKUWA WAKIHATARISHA MAISHA YA WAFANYA BIASHARA WANAO WEKEZA NA KUCHUKUWA PESA KWENYE MABENKI NA HATA WAUZA MAZAO SOKONI. WAONDOLEWE HARAKA KABLA HAWAJA ENDELEA KUHATARISHA UHAI WA WATU NA MALI ZAO.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2013

    Wote mliochangia hapa na issue nzima ya BOdaBoda ni Mazganyanza tupu!!
    Itungwe sheria kali ya mpangomzima wa BodaBoda ikianzia kwa mmiliki mwendeshaji na abiria - juu ya ujuzi-uwezo na uelewa wa sheria za mwendeshaji-barabara-abiria na watumiaji wengine wa barabarani-waendao kwa miguu ama usafiri mwengineo wowote!! La si hivyo tutaendelea kujichanganya-kuumia na kuumizwa pasipo sababu ya msingi!! Waliona wajibu huu ni mimi na wewe unayesoma ujumbe huu sasa. Tuamke - Tuache Lawama na Matusi. Pumbafukabisa!!

    ReplyDelete
  5. Kama kweli tunataka Jiji letu lionekane ni Jiji la Kimataifa na kuwa na hadhi,hebu tuachane na hii biashara ya Boda boda hapa Jijini.DSM hakuna Uhaba wa Usafiri,tatizo liko kwenye Miundo mbinu (barabara) ambapo tunaona jitihada za Serikali ktk kutatua changamoto hiyo.Boda boda ni "KERO"...ni kero kubwa sana jamani.Kuna kila sababu ya kutunga sheria itakayo dhibiti matumizi ya Bodaboda ktk Miji mikubwa.Kwanza mbali na majeraha,Ulemavu na vifo visivyo vya lazima ambapo yote hayo yanatokana na wengi wa waendesha Bodaboda kutokuwa na Elimu ya matumizi ya chombo chenyewe,lakini pia na matumizi ya barabara na Usalama.(kwa vyombo vingine vya moto na waenda kwa miguu)

    Aidha,kwa bahati mbaya sana,Bodaboda imebadilishwa matumizi na baadhi ya waendeshaji,ambapo wamekuwa wakizitumia kwa Wizi na unyang'anyi wa porch za waenda kwa miguu,pamoja na Ujambazi kwa ujumla kwa kuwa ni chombo rahisi kwa kutoroka.

    Natoa Rai kwa Mamlaka husika,pamoja na kuwa ni kisaidizi cha ajira kwa Vijana,lakini tayari ina dosari za kutosha.Boda boda iwe MWIKO ktk miji mikubwa.Zinafaa kwa vijijini ambako kuna changamoto kubwa ya Barabara.Sheria iundwe tuepukane na majanga ktk miji yetu,hasa Dar es Salaam,Arusha,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2013

    Hawa dereva wa bodax2 wanahitaji elimu na sio hiyo tu miundo mbinu hairuhusu. Hata kama wangeweka hizo barabara za boda boda na baiskeli je watu wanajua umuhimu wa sheria TZ kwetu hapa? Aaaa shida tupu inabidi tuanze kufundisha watoto wetu umuhimu wa sheria kwanza! Wasijerithi hii naniiihiiiiii!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2013

    Mimi kweli nashindwa kuelewa hii kampeni ina akili gani. Hii ni hatari kwanini wasifanye kampeni ya kuwaelimisha waendesha bodaboda na kwanini kusitungwe sheria kali ili waogope kuvunja sheria, badala ya kupambana na hatari sasa tunafanya kampeni ili wapate misaada hospitali, kwa nini tusizuie wasiende huko hosiptali? Ingeweza kuanzishwa kikosi maalum cha wana usalama barabarani cha kupamban ana hili tatizo, kweli inamaana miongoni mwetu watanzania hakuna anyeweza kulisimamia hili? Degelavita.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2013

    HATA NYIE WENYE KAMPENI HAMUELEWI SHERIA. KWANINI, MUNAPANDA PIKIPIKI BILA YA HELMET?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...