Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.
Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15 zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).
Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China).
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen Clark Mtendaji Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na menejimenti ya shirika hilo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa UN Women Bi. Lakshmi Puri (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Ludovick S. L. Utouh mara baada ya kikao cha pamoja cha kilichofanyika makao makuu ya Ofisi, mjini New York Marekani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tuvako Manongi (Watatu Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania, New York Marekani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Modest Mero (Watatu Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowatembelea, UN Plaza, New York Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2013

    wachina waindi wamarekani njoni njoeni tanganyika njema njoeni muwekeze hata miaka miaa tutakupeni mikataba njoeni after all kwanini tujali kwani hii nchi yetu tukimaliza miaka yetu ya utawala tunakula kuku kwa mirija na nchi iache iangamiye kama ngaamia

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Bwn Uttoh. Unaonyesha mfano katika kuwezesha vijana kushika majukumu pindi utakapo achia ngazi. Wewe ni mfano wa kuigwa. Bila kuwapa vijana majukumu, kunakuwa na Ombwe la utaaluma na uongozi. Mitafaruku mingi, husababishwa na kukosekana kwa ajira na viongozi vijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...