Mwenyekiti wa TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile pichani akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani} zaidi kuhusiana na maandamano hayo kumuondoa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.
Chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo wamepanga
kufanya mandamano ya kumuondoa mkuu wa wilaya ya kilolo,Mh. Gerald Guninita kwa
madai kuwa anawanyanyasa na kuwadhalilisha watumishi wa umma.
Wakizungumza na
wandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile, wamesema kuwa hawamwitaji mkuu huyo wa wilaya
kutokana na utendaji wake wa kazi kwa wafanyakazi wa umma, kuwa wa vitisho.
Wamesema kuwa kutokana
na kutoa kauli za vitisho kwa watumishi hao wa umma, zimekuwa zikiathiri
utendaji na uhusiano makazini kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa hofu.
Kwa upande wake katibu
wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU ,John Mbingi ,wamewataja
watu ambao tayari wamefanyiwa udhalilishaji na mkuu huyo kuwa ni Thomas Nyambage, ambaye ni afisa mifugo na kaimu wao kata ya Mlafu pamoja
na Beatus Nyato,Afisa usafirishaji kilolo ambao walipigwa
pingu hadharani na kuwekwa ndani na kisha kuachiwa huru bila kufunguliwa
mashitaka.
Aidha amesema tayari
uongozi umeshafanya taratibu za kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za juu
akiwemo mkuu wa mkoa.kutokana na malalamiko hayo mkuu wa wilaya hiyo GERARD
GUNINITA ambaye ndiye mlalamikiwa amekanusha mashitaka hayo na kusema kuwa
hajapata malalamiko hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...