Ndugu na marafiki wote tunawaombeni mjaze petition hii na kuituma kwa kila rafiki ili watoto wetu wanaoishi ugiriki waweze kupata haki zao.Nchi hii bila kupiga kelele huwezi kupata haki yako na huu ni wakati kwa kila rafiki asaidie just to fill this petition. Please just spend your 2 minutes to SUPPORT OUR CHILDREN.
Maelezo kirefu kuhusu petition bofya hapa: http://www.ithageneia.org/en
Usikose kuiforward kwa kila rafiki umjuaye
k.n.y 
(Jumuiya ya watanzania ugiriki)
KAYU LIGOPORA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2013

    Hivi mbona mnapigania haki ambazo hamuwapi watoto wa immigrant wanaoishi Tanzania. Kweli mkuki kwa nguruwe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2013

    Jaribuni kutafuta Wakili apeleke malalamiko yenu kwenye Korti Kuu ya Umoja wa Ulaya. Sisi Wabongo wa huku TZ hawatasaidia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2013

    Jamani rudini nyumbani, Bongo ni nzuri sana siku hizi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2013

    The Greeks are one of the most discriminatory people in Europe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2013

    Siku bodaboda zikipotea mtaani mi ndo nitarudi huko mnakotaka turudi otherwise hapahapa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2013

    Duh!Bado mmekomaa tu kwenye nchi hiyo yenye uchumi wa tia maji tia maji?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2013

    Anzisheni CCM Branches, mbona UK, USA wana matawi, may help - u never know.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2013

    Kayu Logopora !

    Kayu Ligopora !

    Kayu Ligopora !

    NIMEKUITA MARA TATU HAPO JUU KWA MSISITIZO KUTOKANA NA UBISHI WAKO.

    Tumekupigia makelele weeeeeeee tokea siku zile mnarushiwa Mikate ya Msaada kwenye Mapipa na Maboksi, WEWE UKIWA UNABISHA NA KUKATAA KATA KATA KWAMBA MAISHA HAYAJAKUWA MABOVU KIVILE, NA SASA LEO MAJI YAKAKUFIKIA UTOSINI UNAOMBA MSAADA KWA AJILI YA WATOTO.

    JE, HUO NDIO UONGOZI?

    JE, UMEWASILIANA NA SERIKALI NYUMBANI?

    KWA NINI UNAKUWA MBISHI SANA?

    KWA NINI MSIWARUDISHE WATOTO NYUMBANI TANZANIA MBAKIE NINYI WAKUBWA HUKO?

    TAFADHALI OMBA MSAADA WA KUWARUDISHA NYUMBANI TANZANIA WATOTO NA SIO MSAADA ILI UENDELEE KUWAWEKA HUKO KABURINI UGIRIKI!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2013

    Kayu Ligopora wasiliana na Raisi wa Umoja wa Ulaya Jose' Manuel Barroso na sio sisi Watanzania yakwetu yanatushinda ya kwenu Ulaya tutayaweza vipi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2013

    Kayu Ligopora wasiliana na Raisi wa Umoja wa Ulaya Jose' Manuel Barroso na sio sisi Watanzania yakwetu yanatushinda ya kwenu Ulaya tutayaweza vipi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2013

    Kayu Ligopora acha ubishi TEMBEZA BAKULI, WASILIANA NA SERIKALI YAKO NYUMBANI BONGO, PANDISHA NDEGE WATOTO RUDISHA MPIRA KWA 'KIPA' Jakaya Mrisho Kikwete atawapokea Watoto wa Tanzania kwa Ukarimu saaana!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2013

    Watanzania Ugiriki na wewe Kayu Ligopora mna adabu kweli?

    Matatizo kama hayo badala ya kutumia Itifaki zinazo kubalika kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na Serikali yenu kwanza mnakurupuka kufanya Majukumu ya Serikali ninyi wenyewe, sasa huko si ndio kukosa adabu kwenyewe?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2013

    Wewe Kayu Ligopora na wenzako, huko Ugiriki hamna chenu ona sasa mnavyofanyiwa ninyi na watoto wenu utafikiri Uraia wenu upo Likizo!

    Si bora mrudhishIe Pasipoti zenu za Tanzania na kuitwa tena Watanzania kuliko kuwa Wagiriki msio thaminiwa?

    Si bora m renew Kadi zenu za CCM ?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2013

    Wewe Kayu Ligopora na wenzako, huko Ugiriki hamna chenu ona sasa mnavyofanyiwa ninyi na watoto wenu utafikiri Uraia wenu upo Likizo!

    Si bora muwasiliane na Mhe. Raisi Kikwete mrudishiwe Pasipoti zenu za Tanzania, na Kadi za Kupigia Kura na kuitwa tena Watanzania kuliko kuwa Wagiriki msio thaminiwa?

    Si bora m renew Kadi zenu za CCM ?

    ReplyDelete
  15. mutabarukaJuly 23, 2013

    Watanzania mnachukiana namna hii? Hapa nashindwa kuelewa kama mnamchukia kayu ligopola au mnawachukia watanzania wenzenu wanaoishi ughaibuni?....

    ReplyDelete
  16. Jamani watoto wana haki ya kulindwa wakati wote,mahali popote katika nchi yoyote.Kusaini petition ni njia ya kuonyesha concern kwamba haturishiki na yale watotot wanafanyiwa,tusiangalie kwa nini ndugu zetu wapo nje kwa kuwa hata nyumbani tuna wageni na hatuwatesi watoto wao.Petition ni kama maandamano kwa njia ya kalamu na njia yenye nguvu sana katika kudai haki,inatumiwa sana na mashirika kama Amnesty international na imesaidia watu kuachiwa toka vizuizini,ni sauti ya wengi.Hatujui kwa nin wenzetu wapo huko lakini ni maisha ambayo yeyote kati yetu anaweza kujikuta,wametuma petiton kwetu kwa kujua kwamba watapata msaada mkubwa nyumbani.Tusijali ni kwa nini wao hawatusaidii au kwa nini wapo huko,tuwasaidie kwa manufaa ya watoto.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2013

    Hizi sheria zinawekwa ili kufanya uhamiaji kwenye nchi hizi za Ugahibuni unakuwa mgumu. Kuna sheria sasa UK kuwa raia wa UK hawezi kuoa mgeni kama mshahara wake ni kima cha chini. Kama utaoa na una mshahara wa KCC basi mke hatapewa Viza. Sasa nyinyi ishini huko kama walivyofanya Waturuki Ujerumani, waliishi miaka nenda miaka rudi bila ya kupewa uraia hata kama wamezaliwa Ujemarumani.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 23, 2013

    UFAFANUZI KWA WALE WANAOELEWA VIBAYA AU WASIOTAKA KUELEWA
    Petition hii imeandaliwa na SECOND GENERATION 2.0 HAIKUANDALIWA NA KAYU NA WALA HAIKUWALENGA WATOTO WA KITANZANIA,BALI WATOTO WOTE WA WAGENI (hebu tuwe tunasoma kwanza kabla hatujatoa rai zetu)

    Hapa kazi kubwa iliyofanywa na Kayu naona ni kuforward ili zipatikane signatures nyingi duniani na kwa kuwa wabongo wengi wanapitia Michuzi naye ndiyo kaileta hapa.
    Sasa kuna uhusiano gani hapa na KUWARUDISHA NYUMBANI WATOTO WA KITANZANIA?
    KUNA KOSA GANI LA KAYU KUFORWARD HII PETITION?
    Huyu Kayu mimi nimesoma meseji zake nyingi kuhusu wageni ugiriki HANA UBAYA WOWOTE NA ANAJITAHIDI SANA inaelekea kuna watu wana yao ya kibinafsi.


    ReplyDelete
  19. ndio maana Tanzania hatuendelei mtu hata hajasoma kitu kisha analawama tu
    Haki ya Mtoto ni popote tu na hiyo si haki ya Watoto wa Tanzania

    Hivi mbona sisi tunashabikia Mandela apone Mandela muokozi je amekuokoa nin au amekusaidia nini wewe kAMA TANZANIA?

    Naunga mkono sheria hii na nimeshasaini kwa vile najua Uchungu wa watoto kama mimi nina watoto hapo Ugiriki basi naunga mkono ijapokuwa sipo Ugiriki kwa vile najua nini maana ya Mtoto

    Kayu έχετε την υποστήριξή μου

    ABDUL UK

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 24, 2013

    kuna wabongo wengi wanaopitia ukurasa huu wa Michuzi kazi yao kubwa ni KULAUMU KILA HABARI INAYOHUSIANA NA UGHAIBUNI!!
    Inaelekea watu hao hata nje ya mkoa waliozaliwa hawajawahi kutoka kwa hiyo wakiona kuna habari yoyote ya ughaibuni wao huwajia ile jealous na cha kwanza wakifanyacho ni KULAUMU NA KUWATAKA WATU WARUDI BONGO!!
    Hawaelewi na wala hawataki kuelewa kuwa maisha popote duniani yana ugumu na yanahitaji struggling.
    PUNGUZENI CHUKI KWA WENZENU WALIOPO UGHAIBUNI. NAO NI NDUGU ZENU SI MAADUI ZENU.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 25, 2013

    Naomba kuongezea: petition nimei-sign kwani iwapo itafanikiwa, itatetea watoto wa mataifa mengi. Kwa wale wanaofikiri kuwa serikali ya TZ inatoaga mchango kwa wenye matatizo Mie ya nchi hiyo sahau. Kama PR wanaweza kuiweka ktk TV tu.Pia, tuwarudishe watoto TZ waje kids njaa? Hivi Kuna program ya Marlo ya kusaidia watoto? au mnataka waje waoshe vioo vya gari traffic light? Au mnataka kuwalawiti? Wishy: SIO WOTE TUISHIO UGHAIBUNI TUNAA URAIA WA HUKU. blackmpingo

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 25, 2013

    Maisha ya mtu mwingine kama anaishi kijijini, mjini, ulaya au amerika yanakuhusu nini. Komaa na ya kwako. Kama kuna jamaa yako yuko mahali wewe binafsi hupapendi mpigie simu arudi na si kuandika pumba kuhusu mambo ya wengine bila lisechi

    ReplyDelete
  23. Kuna aina mbili ya watu wanaosema "eeeh si mrundi tuu nyumbani kwenu!!!"

    1. Waliojaribu kwenda ughaibuni wakashindwa

    2. Waliowahi kwenda ughaibuni lakini wakashindwa kubakia ughaibuni. Aidha wamerudishwa bongo au maisha yaliwapiga makonzi walipokuwa ughaibuni.

    Makundi yote mawili hayo yanatafunwa na mdudu "jealous".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...