Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania  Mhe. Mussa Zungu Azzan akifungua kikao cha Kamati tandaji pamoja na  Sekretarieti jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 44 wa  CPA Kanda ya Afrika utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto kwake ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa CPA Bwana Demetrius Mgalami. Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mkamu wa Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa CPA Kanda ya Afrika.
 Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti
 Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Kilindi Mhe. Beatrice Matumbo Shelukindo akichangia wakati wa mjadala. 
Wajumbe wa CPA Tawi la Tanzania (Na Prosper Minja - Bunge)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...