Dawasco imezindua rasmi Mfumo wa Malipo ya ankara za Maji ulioanza rasmi kutumika Tarehe 01.07.2013 Katika vituo vyake vyote 13. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha huduma kwa Mteja.
Pia mfumo utasaidia kupunguza msongamano wa muda mrefu uliokuwepo wa kulipia Madirishani na utampa mteja njia mbalimbali za kulipia Bili yake na kwa wakati wowote.
Mfumo huu pia utamsaidia Mteja kufanya malipo sehemu yoyote nje ya Jiji la Dar es salaam na hata nje ya Nchi
Malipo kwa njia ya Benki yatafanyika kwenye tawi lolote katika Benki zifuatazo: CRDB – A/C No. 01J1021921900, BARCLAYS- A/C No. 0014003711, BANK OF ( BOA) –A/C No. 02022460009 na NMB No. 20103300047
Mteja atakwenda Benki anayotaka kufanya Malipo na kujaza Fomu ya fedha (deposit Slip). Mteja ahakikishe ameandika namba ya account ya Dawasco kwa usahihi ikifuatiwa na kiasi cha fedha anacholipia, kisha kurudisha fomu kwa karani wa Benki kwa Malipo.
Huduma za kibenki kwa kutumia simu za kiganjani ni kwa Wateja Wenye Akaunti Katika Benki za; CRDB, NMB, BENKI YA POSTA, AKIBA COMMERCIAL BANK (ACB) Na EXIM BANK.
Malipo kwa kutumia Simu ya kiganjani yatafanyika Kupitia M-PESA, AIRTEL MONEY, TIGO PESA, Na ZANTEL EZY PESA.
Pia malipo kwa ankara za Maji zinafanyika kupitia ATM ZA UMOJA SWITCH, huduma ya SELCOM na MAXMALIPO inayopatikana kwa Mawakala waliopo kila kona ya Jiji La Dar Es Salaam.
Aidha kuna matawi ya Benki yako karibu na vituo vya Dawasco hivyo wateja wa maeneo husika watapata urahisi wa kufanya Malipo yao ya kila mwezi na kuondoa usumbufu wa kwenda mbali zaidi.
Matawi hayo ya Benki yaliyo karibu na Vituo vya Dawasco ni haya yafuatayo: Kituo cha Dawasco Temeke kilichopo Temeke Usalama kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Temeke Hospital, CRDB – Quality Centre
Kituo cha Dawasco Kawe kilichopo njia panda ya Kawe kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB yaliyopo Mbezi Beach, Kijitonyama, Mikocheni na Mlimani City na matawi ya NMB yaliyopo Mlimani City, Mbezi Beach na Mwenge na Tawi la BOA Bank iliyopo Sinza
Kituo cha Dawasco Tabata kilichopo Dar West kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB Tabata Magengeni.
Kituo cha Dawasco Kimara kilichopo kimara mwisho (Matankini) kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Ubungo Mwisho, CRDB-Mbezi Stand Mpya, CRDB-Mlimani City, NMB, BANK OF AFRICA (BOA) zilizoko Ubungo Plaza, CRDB Ubungo Stand, ATM ZA UMOJA SWITCH-zilizopo Mbezi Suka
Kituo cha Dawasco Kinondoni kilichopo nyuma ya jengo la Airtel kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB- Namanga/Msasani, ATM ZA UMOJA SWITCH- Mwanamboka, AKIBA COMMERCIAL na CRDB zilizopo Millenium Tower Makumbusho
Kituo cha Dawasco Magomeni kilichopo Magomeni Mapipa kipo karibu na Matawi ya Benki ya BARCLAYS- Magomeni Mapipa na NMB-Magomeni Mikumi.
Kituo cha Dawasco City Centre kilichopo Kisutu kipo karibu na matawi ya Benki ya EXIM BANK-Morogoro Road eneo la Fire na CRDB-Lumumba.
Kituo cha Dawasco Ilala kilichopo Boma jirani na Mwalimu House kipo karibu na Matawi ya Benki ya BOA-Amana, NMB-Boma, Barclays-Buguruni Malapa, AKIBA COMMERCIAL BANK-Mtaa wa Uhuru na Likoma, CRDB-Lumumba, Mnazi Mmoja na Mtaa wa Uhuru.
Kituo cha Dawasco Kibaha kilichopo karibu na Ofisi za TRA kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB-Kibaha na CRDB-Kibaha
Kituo cha Dawasco Mlandizi kipo karibu na Matawi ya CRDB na NMB
Kituo cha Dawasco Bagamoyo kilichopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Bagamoyo na NMB-Bagamoyo
Kituo cha Dawasco Gerezani (Makao Makuu) kilichopo karibu na jengo la Water Front kipo karibu na Matawi ya Benki ya CRDB-Water Front, NMB-Samora.
Kituo cha Dawasco Boko kipo karibu na Matawi ya Benki ya NMB na CRDB jengo la Kibo Complex, ATM ZA UMOJA SWITCH zilizoko eneo la Africana.
LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA WAKATI WOWOTE
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO MAKAO MAKUU
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala (Kulia) na Meneja Uhusiano Bi. Irene Mkene akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla wakati wa uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam
Wawakilishi wa mabenki katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam.
Wawakilishi wa mitandao ya mawasiliano katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...