Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja ( suti nyeusi)akimkabidhi Zawadi ya Kikapu Kamishna Mkuu wa
Magereza wa Zambia, Percy Chato. Kikapu hicho kimetengenezwa na Wafungwa wa
Gereza Kuu Ukonga. Hafla fupi ya kuwakaribisha Wakuu wa Magereza
Nchini toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika imefanyikia
katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es
Salaam
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja akitoa hotuba fupi wakati wa hafla aliyowaandalia Makamishna Wakuu
wa Magereza Nchini toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika.
Hafla hiyo imefanyikia katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia
Magerezani, Ukonga Dar es Salaam
Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Magereza Nchini Namibia, Bi. Feris akitoa
neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir
Minja(Suti nyeusi)kwa kuwaandalia hafla hiyo fupi pamoja na kupata fursa ya
kubadilishana mawazo ya namna ya Uendeshaji wa Magereza. Hafla hiyo imefanyikia
katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es
Salaam
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(Suti nyeusi) akiwa na Makamishna Wakuu wa Magereza kutoka Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika katika hafla fupi aliyowaandalia
baada ya kumaliza Kikao cha Mawaziri wanaohusika na Ulinzi na Usalama toka Nchi
za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika( wa kwanza kushoto ni
Kamishna Mkuu wa Magereza wa Zambia, Percy Chato, ( wa pili kushoto) ni
Kamishna Mkuu wa Magereza wa Msumbiji, Dkt. Eduardo Sebastiao, (wa tatu
kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Tom Moyane, (wa kwanza
kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Malawi, Naibu Kamishna wa Magereza,
Ms. Phiri, ( wa pili toka kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Namibia,
Kamishna wa Magereza, Ms. Feris. Hafla hiyo ilifanyikia katika Viwanja vya
Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga, Dar es Salaam
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu
wa Magereza toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(Wote
waliokaa), Wengine waliosimama ni Maafisa wa Jeshi la Magereza ambao
wameongozana na Makamishna hao pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi toka
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza . Hafla ya kuwakaribisha imefanyikia leo
katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es
Salaam
Kikundi cha Sarakasi kinachoundwa na Askari wa
Jeshi la Magereza wakionesha umahiri wao katika hafla ya kuwakaribisha kama
unavyoweza kumuona Askari wa Kike ambaye alikonga nyoyo za Makamishna Wakuu wa
Magereza toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...