Mara nyingi Madereva wengi wa Magari ya Masafa marefu hupenda kuweka matawi ya miti mabarabarani pindi wapatapo matatizo kwenye magari yao ikiwa ni kama ishara ya tahadhali kwa magari mengine yatumiayo njia hiyo,lakini utaratibu huu umekuwa ni mbaya sana hasa pale ambapo gari husika likiwa limepona na kuondoka katika eneo hilo.kwani matawi haya huachwa hapo hapo barabarani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2013

    Nchi gani hiyo Tanzania?? aaahhh mbona hiyo sawa tu tena kawaida sana, Desturi yetu huwa tunasafisha pale tunapotarajia ugeni tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2013

    Ingawa ni uharibifu wa mazingira..naaunga mkono huo utaratibu. Kwa wasafiri wa kila mara watakua wananielewa..utaratibu huu unakoa maisha sana,vitriangle hua havitoshelezi. Ila ni vizur wakayaondoa pindi gari linapopona ili njia zote mbili ziwe wazi magar yapishane kwa ukawaida

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2013

    Imekaa kwenye lami

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2013

    watanzania ni zaidi ya wanyama maana hata paka hufukia kinyesi chake... wazungu wana haki kutuita NYANI...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2013

    Alama za Tahadhari za Ki Afrika. Hatari ikidhibitiwa, alama zinabaki ili kuleta Hatari ingine. Kwani wewe unauliza Jibu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2013

    Picha ya Lini? Nimepita hapo kwenye basi jumapili 30/06 nilioona. Nadhani ukikaribia Segera ukitoka DAR.

    Alama hizo zina kazi. Nilipata hadithi kule Songea kwamba kulikuwa na dereva mmoja matata sana kwa askari wa usalama, nasikia sasa ni marehemu. Ameshawahi kuangusha gari lakini kwa kuwa hakuwa na mwendo mkubwa polisi walipofika wakamkuta hashikiki akijifanya amelaza makusudi ili aitengeneze.
    Yaani huyu bwana alikuwa matata kweli na waangalizi wa sheria za barabarani. Siku moja aliharibikiwa akasimamisha gari na kulitengeneza bila kuweka alama yoyote. Basi ikaja gari nyingine ikaligonga gari lake, kesi ikawa kubwa kiasi cha kupelekwa mahakamani. Yule jamaa aliegonga gari ya dereva wetu machachari akajitetea sana kwamba aligonga kwa kuwa barabara hakukuwa na alama yoyote. Gari lililoharika halikuwekewa hata alama ya tawi la mti? Kama kawa dereva wetu machachari akapata upenyu unaosemekana ndio aliotokea! Akasema. Mheshimiwa hakimu kama huyu bwana nimesimamisha gari hakuliona, hivi tawi la mti angeliona kweli? si angenigonga tu!?
    Matawi ya miti yanasaidia lakini ni uchafuzi na uharibifu wa mazingira ikiwa pamoja na ukataji hovyo wa miti yenyewe. Tutumie kwa tahadhari.

    sesophy03@gmail.com

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2013

    Watanzania wengi ni wavivu kufikiri. Ndio maana tunaishia kulalamika eti wanaajiriwa wageni tu. Sisi wenyewe tunajijua kuwa hatunazo. tunaangalia usawa wa pua basi.

    We tazama mtu anaweka tawi barabarani wakati wa shida, shida ikisha anasahau kuweka mambo sawa. Ndio maana hata ajali haziishi kumbe wanaoendesha magari matajiri vichwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...