Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2013

    Hongera Raisi Kikwete kwa Hotuba ya matumaini makubwa kwetu wananchi.

    Mweleze Brother Big Obama atuletee DRONES (Madege yasiyo na Marubani)ili tukabiliane na Maadui zetu ambao wengi moja kwa moja ni Majirani zetu.

    Hebu angalieni ktk kule Darfur Majeshi ya Kulinda Amani yanajumuisha nchi nyingi sana lakini Mashambulizi yanatokea Maafa yanaangukia Wanajeshi wa Kitanzania peke yao!

    Kule Kusini ziwa Nyasa yle mama analeta fyoko fyoko, mbona Maraisi waliotangulia hawakuwa na sera anazozileta yeye ?

    Hakuna Jinsi tupo pamoja Raisi Kikwete tutakula nao Maadui sahani moja na tutailinda nchi yetu hadi dakika ya mwisho!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2013

    Congratulations Mh.rais JK...well said...message sent and delivered!!!hukusukutua wala kumung'unya maneno...umehit kwenye point PK ajaribu atapigwa kama alivyopigwa Idd Amin - RIP...Mh. rais tuko pamoja kwa hili...nchi kwanza vyama baadae!!message sent...and delivered!!!
    Mdau wa Oxford..UK.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2013

    Hongera sana mh raisi wetu MSG tumepata

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2013

    Mungu ibariki Tz,Big up JK maana umeongea mchana kweupe ukasikika na kueleweka.Tuko nyuma yako mkuu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2013

    Mh Rais message sent! Hebu tusubiri kama kale mutemi ka ile wilaya ukivuka mto (yule Kananihiinoo bwana na nyie:-) kama amemusikia Rais wa Ma-Rais alivyongea. Hebu mu m fowardie haka kaujumbe jamani kasije kuongepea umma wake kuwa hakakuupata.lol

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2013

    Nia ya kumpiga tunayo..sababu za kumpiga tunazo na uwezo pia wa kumpiga na kumsambaratisha tunao....hongera sana mheshimiwa rais kwa hili, tuko pamoja sana kikazi zaidi...huyu PK hawezi kututukania rais wetu hivi hivi,whos that guy??...na ajaribu tu asalaalah tutampiga kama ilivyokua kwa Idd.....message sent and delivered!!! mh. rais tuko pamoja nchi kwanza upinzani baadae!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2013

    Hivi hii message delivered ni kwa nani? Mbona mumenicha kwenye mataa?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2013

    Nimefarijika sana na neno hili tu, Hatuna nchi nyingine isipokuwa hii, welldone Mhe: Rais leo umetuosha uso, nchi yetu haiwezekani tuwe na majirani maadui, tupambane nao mpaka mwisho, ili tuweze kuwa salama, atakayeleta choko choko tutamshughulikia mara moja, raia wanataka kulala usingizi kwa amani, ndy tanzania tuliyoizoea! mungu ibariki Afrika, mungu Ibariki Tanzania, Ameen!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2013

    sielewi ni nani anachezea TZ kuna vita au????????

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2013

    Tuko nyuma yako Mr. President. We will fight to our last blood for our country. Mungu Ibariki Tanzania. Mdau Kyela..Kasumulu Border

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2013

    Dikteta PW na marafiki zake majirani ujumbe wameupata kwetu watanzania PW ni sawa na mwiba wa kijiwe ndani ya kiatu lazima utolewe ukiendelea kuleta maumivu usije ukaleta madhara makubwa kwa tamaa zake za kundelea kuwepo madarakani na kutawala daima zidi ya kukaa mezani na wapinzani kutafuta misingi ya amani kwa nchi.
    Watanzania tunataka muungano wa amani kwa jimbo la ziwa mashariki kuleta mandeleo ya kiuchumi.
    PW hayupo peke yake ana marafiki nchi jirani kwa ujumbe wa raisi JK na Afande Mkuu wa Majeshi utakuwa umewafikia.
    Watanzania wapo salaama bila khofu tena zidi ya shughuri za kawaida za kiuchumi na kujenga taifa.
    PW akipanua mdomo wake tena kuichafua hali ya hewa safi na usalama ndani ya Tanzania basi afande mkuu binafsi ampelekee basketi ya maua na kuwapa pole kwa "genocide" iliyotokea nchini kwake miaka michache iliyopita asijaribu tena kuyatafuta mahafa mengine zaidi ya hayo yaliyowakuta.
    Iddi Amin aliachiwa kijidirisha cha kutokea na kukimbia hakurudi tena waganda na watanzania kukawa na malewano ya amani na kutoingiliana kisiasa.
    PW hatokuwa na dirisha la kutokea na hatokuwa na shimo la kujichimbia,wala nchi jirani pakukimbilia.
    Tanzania tutaishi kwa amani bila ukabila na tofauti za kidini.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2013

    HATUNA NCHI YOYOTE NI HII HII, NI MESSAGE NZURI SANA, KWENU NI KWENU, NA PAKO NI PAKO , PAPIGANINIE KWA GARAMA YOYOTE ILE, USIPACHE PAKUTOKE, KUPARUDISHA NI KAZI, NA MKAATAA KWAO NI MTUMWA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2013

    Mhe Rais wetu amefanya vizuri sana kueleza mipaka ya uvumilivu wetu hongera sana. Nimeona pia mapigo ya Manonge kule Umoja wa Mataifa huyo sasa ndio size ya kujibishana na hako kadudu PK mnakokataja.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2013

    Hongera rais message delivered to Malawi and Rwanda wanaojaribu kucheza na Tanzania Siku zote huwa ukweli unauma ni kweli kagame ndie mwenye majeshi ya M23 ndiye anayevuruga amani ya DRC nani asiyejua watu kama kagame hawatakiwi kwenye jamii Kagame chezea kongo lakini usicheze na TZ tutakupa kichapo na hao m23 wako. Tanzania oyeee taifa kubwa hili moto wakuotea mbali mungu bariki nchi yetu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2013

    Hongera raisi ujumbe umefika kwa Malawi JB na Kagame. Nani asiyejua kuwa kagame ndiye mwenye majeshi ya m23 ndio maana amekasirika baada JK kusema ukweli siku zote ukweli unauma. Wee kagame usicheze na Tz nafikiri unaijua vizuri Tz sasa chunga tena chunga Tanzania taifa kubwa Tanzania oyee mungu bariki nchi yetu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2013

    he he he he he jamani msishabikie vita. vita yaua jamani mjue vitambi vyenu hivyo vitafumuliwa lol. shauri yenu endeleeni kushabiki vita maana hamna aijuae vita hupendelea vita. naomba braza misupu usibanie.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 27, 2013

    Tunakupongeza kwa huo ushujaa wako rais wetu. Ila na ile ya ndani ya nchi watu kumwagiwa tindikali na pia watu kupigwa risasi hapo Dar na kwingineko nayo mheshimiwa ungeyazungumzia ili wanaofanya hivyo wapate ujumbe wao toka kwako ili wasiendelee kutesa wengine bila sababu yoyote ile katika nchi nzuri ya Tanzania yenye amani tele.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2013

    Mkuu wetu ujumbe umefika ila tunaomba vita iwe last resort kwa sababu vita hata kama utampiga adui yako madhara yake ni makubwa.
    Nanukuu maneno katika wimbo wakati wa vita vya Uganda. "Vita siyo mchezo, vita si lele mama; vita ni watu kufa, na mali kuteketea."

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 29, 2013

    Obama ameshampigia simu PK mara kadhaa na akamwonya kuhusu hakati zake Mashariki ya Congo DRC.

    Atalala Kigali ataamshwa na milio ya Madege angani ata twangwa vikali!

    Chezea Marekani weye?

    Kama atafanya mchezo awaulize Iraq na Libya ni nini kiliwapata?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2013

    PK cheza mbali na TZ Tanzania ni Taifa Moja Taifa linalo elewana. Wana Raisi mwenye upeo Busara,Hekima NK.....PK wakikuijia wewe utakimbilia wapi?Uganda watakuijia,Congo ndo kabisa huwezi kwenda, South Africa huwezi,Zimbabwe huwezi Malawi huwezi Zambia huendi.Sasa wewe PK utaenda wapi? Hapa USA hatukutaki Uraya nako hawataki kukusikia pole sana ndungu yangu usije ukawa Kama Gadaffi.
    ,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...