Na Angela Sebastian,
Bukoba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema udhaifu na uzembe unaoendelea kufanywa na watendaji wa Idara ya Uhamiaji umesababisha nchi kuwa na lindi kubwa la wahamiaji haramu kutoka katika nchi zinazotuzunguka.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kwa uchungu leo Ikulu ndogo mjini Bukoba wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani hapa na kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kwasasa Tanzania ina wahamiaji haramu zaidi ya 52,000 huku mkoa wa Kagera ukiwa na wahamiji haramu zaidi ya 36,000 ambapo ameongeza kuwa hilo ni tataizo kubwa lililosabaishwa na udhaifu wa watendaji wa idara ya uhamiaji na litaigharimu nchi yetu.
“ Tanzania sio shamba la bibi kila mtu anaingia na kutoka na mifugo yake eti kwasababu kuna sehemu nzuri ya malisho alafu watendaji wa vijiji na wenyeviti wanawapa vibari wahamiajia hao na kuwahonga viongozi hao wa vijiji ng’ombe sana sana hawazidi wawili na nyie uhamiaji mnaona na kuyafumbia macho mnatenda dhambi kubwa asambayo inapeleka nchi yetu katika hali mbaya kwa kipindi cha miaka 50 ijayo”alisema Rais Kikwete kwa uchungu.
“Hili sijalisema kwa mara ya kwanza,niliisha lisema hata mwaka 2008 nilipokuja Kagera na kuhutubia wilayani Muleba lakini bado mmenyamaza,kuna mtu anaitwa Katongole anaishi kule mpakani Mutukula ndiye anayeingiza wahamiaji hapa nchini ameishajua bei zenu anawahonga anaingiza watu wake,mtu anayetoa rushwa anajulikana ushahidi upo wanaohongwa wanajulikana PCCB mnafanya nini mmenyamaza tu basi kazi imewashinda”aliongeza Rais
Alisema hili suala la watendaji na wenyeviti wa vijiji kuwapa vibali watu hao,uhamiaji wanalijua na wameliacha kwa muda mrefu na kama wangelitilia maanani pale mnapobaini kuwa viongozi hao wametoa vibali feki mnawakamata na kuwachukulia hatua,nchi isingefikia hatua hii ya kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji kiasi hiki.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya ulegevu na udhaifu wenu inawafanya watu wajiulize maswali mengi juu ya utendaji wenu wa kazi na kuwaona kama nyie ndio sehemu ya tatizo; kila siku sisi misako tu mpaka lini?kwanini tusisimamie zoezi hili kwa umakini pale mtu anapoingia tu na kumbaini tunamrudisha mara moja na sio kusubiri wawe wengi ndio mfanye misako,itafikia siku mtataka kuwarudisha watagoma na kukuelezeni kuwa ni kwao na wanahaki ya kuishi hapa jambo ambalo litazua mtafaruku mkubwa kati ya wazawa na hao wahamiajia haramu na mwisho wake ni mapambano.
Alisema hatuchukii wageni ila mtu anayetaka kuishi Tanzania afuate utaratibu,apeleke maombi uhamiaji na watayafanyia kazi na pale mtu akikataliwa kupewa uraia asihoji kwasabu sio kila mtu atapewa uraia kuna wengine ni majambazi,wauza madawa ya kulevya na makosa mengine hatuwezi kuwapa uraia”mwaka 1982 Hayati mwalimu Julias Nyerere alitoa uraia wa fursa kwa wahamiaji 30,000 wakapata uraia na mimi kwa kipindi cha uongozi wangu nimetoa Fursa hiyo ambapo watu 160,000 wameomba na kupewa uraia kwaiyo ambaye hakuomba huyo hataki kuwa raia wa Tanzania wasakwe na kurudishwa kwao pia kumbuka hao ni binadamu wasiswagwe kama mifugo kama mtu ana mali yake auze na kuondoka msiwadhulumu.
Aidha Rais amewaasa Watanzania kuacha kutumiwa na watu wenye nia mbaya ya kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kupitia njia ya udini na siasa kwani matokeo yake ni kugawanyika na kupoteza malengo yao.
Pia ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Bukoba kumpa jibu haraka kuhusu wananchi 800 wa mgogoro wa viwanja wanapewa lini.
Well said Mr President. Nashauri tuanzie ktk makampuni makubwa ya simu za mikononi kwani halo ilivyo si kawaida. Karibu kila kampuni Ina wageni zaidi ya 100 eti ni watalaamu. Halo hii inatia mashaka Sana kwa vipi walipunguza wazawa na kuongeza wageni!? Kwa baadhi ya makandarasi Wa hizi kampuni yani ni kichefuchefu utakuta ofisi nzima wamejaa watu zaidi ya 100 hasa ile ya pale mlimani city na ile ya pale makumbusho na ya Morocco,ukiingia utastaajabu utadhani sio Tanzania. Nafurahia kupata watalaamu lakini sio kwa dizaini hii.
ReplyDeleteHivi utaratibu wa vibali ukoje? Maana nahofia vinaweza kuisha ndani ya miaka michache ijayo kama halo itaendelea hivi.
Nawakilisha
Vibali vya kazi vinapaswa kutolewa kwa ujuzi ambao haupatikani kwa watu wetu,sasa nashangaa ni ujzi gani ambao sis hatuna, marketing, It au nini,mbona watu wazuri wapo kibao katika fani hizo.Jamani mngejua nchi za wenzetu ilivyo vigumu kupata kibali cha kufanya kazi, serikali ingepitia upya na kuangalia taratibu , hasa hizi rushwa ndo zinaleta hayo. Mfano hata passport za Tanzania inasemekana zipo na wanigeria kibao na wakifanya majanga utasikia mtanzania, hata hatuaminiki tena kama zamani kwa sababu ya njaa za watu wa uhamiaji. Na Rais kama anayajua yote hayo atoe amri na maelekezo kazi ifanyike siyo kusema watu wanakula rushwa bila kunawa,na kwa nini wanawe kama mabosi wao wanakula pia kunawa?
ReplyDeleteHahahha, ni mlo wa watu hapo hivyo vibali, nchi imeoza
ReplyDeleteNdugu zangu watanzania tumelelewa Kuwa wazembe, wavivu, na wezi. Mimi nilishawahi kuwa mwajiri nikiwa na kampuni ya nje. Watanzania walitushinda kutokana na wizi, uzembe, na uwezo mdogo wa English. Mwishowe nafasi nyeti zote zilipewa watu wa nje. Kampuni za nje wako pale for business, na ukumbuke business sio mchezo kama siasa.
ReplyDeleteMsemo wa vijana wa siku hizi " nchi inauzwa kisailensa" Hali ya wazawa kukosa ajira tanzania imeitengeneza yenyewe.
ReplyDeleteUkifika kwenye makampuni yanayoitwa ya wawekezaji, utakuta wageni wengi sana mpaka wafagiaji. Nenda kwa makampuni ya kichina hapo ndo mtu unashindwa kushangaa. Yetu macho.
Mh Raisi, Kama hao uhamiaji wanafanya uzembe basi wafukuze kazi. Usisahau kwamba wewe ndio kiongozi unayetakiwa kutoa mwongozo na kuwafukuza kazi wazembe. Inakuwa kama una-negotiate na wazembe? Kwa nini mzembe aendelee kushika nafasi ya uongozi?
ReplyDeleteHapo raisi watanzania wote tupo nyuma yako ajira za vijana wa wachuuzi wa biashara za ngazi za chini pia zimepotea na wahamiaji
ReplyDeletemsako uanze haraka majumbani hata barabarani sawa na ughaibuni ni hatari kuwa na mseto wa wahamiaji feki wataidhuru nchi kwa kutumiwa na maadui zetu.
mikidadi-denmark