Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika nyakati tofauti  ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2013


    "UNITE EAST & CENTRAL AFRICA"

    NI vizuri rais Dkt.Kikwete kukutana na Prof.Lipumba kujadili katiba na maendeleo ya taifa pia wasisahau kuzungumzia binafsi wapi Pro.Lipumba anaipeleka CUF wakati sera zake zinakubaliana na za CCM hawaoni sasa umefikia wakati wa bara kujiunganisha kutuletea serikali ya mseto,tuwezu kupiga hatua kubwa ya kufikia umoja wa jumuia ya nchi za mashariki na kati ndani ya bara la afrika.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2013

    Umekutana na mdini mwenzio Lipumba mjenge mikakati zaidi ya kuipasua nchi kwa sera zenu muumiani za udini.Lipumba hana haiba ya usomi wala uongozi ndiyo maana hakubariki na watanzania kwa uwingi wao dhamira yake mbaya kama sura yake!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2013

    watu wengine bhana hapa din imetoka wapi yy kaenda kama kiongozi wa chama fulan dini imetoka wapi jama watanzania kwahiyo mh mbowe akiwa ikulu akakutana na mrema au mbatia anakuwa mkabila au mdini kwa kuwa ni din moja au kabila moja watz watch uot wapi tunaenda jaman hoja za ufivyuuu waakili zetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2013

    Hana sera yeyote Lipumba zaidi ya udini. Udini jumlisha udini ni Udini kwenda mbele.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2013

    Anonymous wa pili unaweza kutufahamisha hasa nini maana ya MDINI AU UDINI? Halafu ueleze kulingana na maana uliyoitafsiri kwa hao watu wawili: lipumba na kikwete.

    Ninavyofahamu miye udini au ukabila maana yake ni kutoa upendeleo katika dini au kabila ambalo huyo mtu anajinasibu nalo kwa makusudi na kudhoofisha makabila au dini zinginezo.

    Mwandosya alisema bungeni kuwa raisi kikwete si mdini kwa kuwa wasaidizi wake wote pale ikulu ni wakristo.

    Kwa maneno haya ya mwandosya anamaanisha kwamba kama wasaidizi wake wote wangekuwa waislamu basi kikwete angekuwa anaitwa mdini. Je, na wewe anonymous wa pili una "DEFINITION" ya neno "UDINI" kama aliyokuwa nayo mwandosya???

    TAFAKARI NDUGU na usome sana vitabu mbalimbali kujua "REALITY". Na ujitahdi kuwa na "OPEND MIND"; lakini kinyume chake hutofahamu mengi yaliyo ya uhalisia katika dunia hii na utaishia jahanam

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 20, 2013

    Cut ur nonsense u looser..we r in 21st century nd u talking rubbish.. get life .. people are awake..no more lies

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2013

    Anonymous wa pili naona unaleta hoja isiyoeleweka. Huyo lipumba ni kiongozi wa CUF na kikwete ni mkuu wa nchi. Kwa kiongozi wa CUF kwenda kwa mkuu wa nchi kueleza yale ambayo kwa mtazamo wa CUF ni muhimu kwa mustakbali wa nchi yetu kuna tatizo gani??? Badala ya kuuliza nini hasa kiongozi wa CUF alienda kwa mkuu wa nchi? Nakumbuka hawa CUF walitaka kuandamana Juni 29, 2013; walisitisha badala ya kuambiwa raisi atakuwa BUSY kipindi hicho. Na kama sikosei wanataka kuandama tena; huenda walikuwa wanalizungumzia hilo; hasahasa kuelezea yale yaliyokuwa yanajiri kule Mtwara. Sasa unataka kiongozi wa chama afanyaje???

    Nchi inajengwa na mawazo yanayofanyiwa kazi. Sasa ulitaka kiongozi gani wa CUF angeenda kumwona mkuu wa nchi? Au muislamu hatakiwi kumwona mkuu wa nchi au kuwa mkuu wa nchi??? Concept hiyo umeitoa wapi kama si ubaguzi katika nchi tunayopinga kila aina ya ubaguzi.

    Ngoja nikuweke sawa wewe ndugu:

    Moja: Ardhi ya Tanzania ni ya Watanzania wote (wabaniani, wahindu, wakrsitu,waislamu,wanaofuata dini isiyofahamika,makabila yote,wasio na makabali,na binadamu wengine wote wenye haki ya kuitwa watanzania). Kwa hiyo tutabanana hapa hapa, ndipo petu.

    Mbili: Watanzania wote wanahaki ya kuwa viongozi/kufanya kazi, n.k.

    Tatu: Mtanzania yeyote anatakiwa atende haki kwa kiumbe yeyote yule kulingana na sheria inavyosema. Hata mbwa au paka au sisimizi apewe haki yake kulingana na sheria.

    Nne: Udini maana yake ni kumbagua mtu mwenye dini nyingine kwa kupindisha haki; iwe kwa kujitungia sheria yenye ubaguzi n.k.; kama ilivyokuwa afrika ya kusini.

    Kwa hiyo ni wajibu wa kila mmoja kufikiri vyema, SIO BLAH BLAH na kuja na SCIENTIFIC FACTS kwa ajili ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2013

    lakini weee michuzi maoni mengine ya watu tunakuomba usiyatoe maana yanatutapisha. kama sheitwani hapo juu sasa udini unahusu nini aulize dunia lipumba nani ataambiwa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 20, 2013

    lakini wewe michuzi mbona commets zangu nikizungumzia ukatoliki bongo huzitoi? lakini wehu wengine wakitukana uislamu huwa unatoa commets zao.

    ReplyDelete
  10. Mdau wa pili hizi siyo comments za kuweka bila kuthibitishwa!

    Je unaweza kututhibitishia hayo unayoyasema au umeamua tu kujifurahisha? nadhani huwatendei haki wasomaji wako ukitoa habari ambazo ili ziaminike zinahitaji kuthibishwa na wewe unaziweka bila huo uthibitisho!
    Hujatutendea haki.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 20, 2013

    HUU NDIO DEMOKRASIA HALISI, TUNAMJUA LIPUMBA NI MDINI NA ANABAGUA WATU KWA UDINI! KAMWE HATAWEZA KUSHIKA MADARAKA YOYOTE NDANI YA TZ, UNAJUA KWANINI?
    KWASASABU WATANZANIA WOTE SI MKRISTO, MUISLAMU,MHINDU,WAPAGANI, NK - WOTE TUNAJUA TULIPOTOKA..TANZANIA IMEJENGWA KWA MISINGI YA UPENDO, KUSTAHIMILIANA,KUHESHIMIANA.
    NI VIKUNDI VICHACHE VYA KIDINI VYENYE SIASA UCHWARA ZAKUBAGUA NDIO WANAFIKIRI WATAWEZA KUINGIA MADARAKANI AU KUWA NA SAUTI NDANI YA UMMA KWA KUBAGUA, KUCHOCHEA CHUKI NDANI YETU!!
    KIONGOZI BORA NA MAANA HUONGOZA JAMII NA WANANCHI WAKE KWA KUWAUNGANISHA WOTE BILA KUJALI WEWE NI DINI GANI, KABILA GANI,ASILI GANI>
    WANASIASA UCHWARA NA WANAOJALI MATUMBO YAO NDIO HAO WANAONGOZA JAMII NA WANANCHI WAKE KWA KUWAGAWA
    NA KUCHONGANISHA KUPITIA UDINI, UKABILA, NK.
    WATANZANIA SASA WANAJUA MENGI, ILA WANAKAA KIMYA, KWANI TWAJUA LIPUMBA NA UDINI WAKE ATAISHIA KUZUNGUKA "UANI" KWA ILA NDANI YA "NYUMBA" YA FAMILIA YENYE WATANZANIA WOTE ISIYO BAGUA MTU KUPITIA DINI, UKABILAM ASILI, KAMWE LIPUMBA HATAINGIA.
    NA SIYO LIPUMBA TU, KUNA AKINA MCHUNGAJI MTIKILA..WOTE NI WABAGUZI.
    NASEMA HAMTUDANGANYI HATA KIDOGO, WADANGANYENI WENZENU WENYE UPEO FINYU FINYU. ILA WATANZANIA WENGI UPEO WAO WA KUFIKIRI NI MKUBWA.
    WAWEZA KUWA NA AKILI ZA DARASANI, UKAWA DAKTARI, PROFESA, MCHUNGAJI, SHEHE, NK - ILA KAMA HUNA UPEO WA KUFIKIRI NA KUTENDA, BASI WEWE NI HUNA MAANA HATA KUJIONGOZA MWENYEWE HIVYO HATA KUONGOZA JAMII HUFAI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 23, 2013

      enyi mnachochea udini mnataka nini ktk nchi hii udini walipumba uko wapi.

      Delete
  12. AnonymousJuly 20, 2013

    Analyzing a book through its cover!!! Is it a proper way? Hapa tatizo ni Uislamu wa waliokutana na kamwe sio uwezo wao kiutendaji, hii ni hatari sana.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 20, 2013

    Mdau wa pili hapo juu udini wa lipumba na kikwete ni upi? eleza tuelewe Otherwise hizo ni propaganda tu za kanisa kuchafua kila kiongozi wa dini isiyokuwa yenu ili ashindwe kutawala kama mlivyosema nchi haitotawalika?nyaraka za kanisa zinazoelekeza wakristo kuiunga mkono chadema na kutoviunga mkono vyama vingine mnafikiri hatuyaoni? ni kina nani wanaosababisha vurugu ktk nchi hii kwa mgongo wa kukingiwa kifua na kanisa kama sio chadema? nani aliyekwambia lipumba kama mwanasiasa yeye basi hana hisia za dini yake? safari hii imekula kwenu maana kwa sasa nasi tunapiga hatua mlizoea kubebwa na serikali, jamii nyengine nao wameamka sasa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 20, 2013

    Kawaida mwenye akili finyu huwa hajijui mpaka zitakapopanuka, lets us give him time atakuja kujua utumbo wake baadae akikua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...