Washindi wa zawadi za Utendaji uliotukuka 1434 kutoka kwa Wanataaluma wa Kiislam Tanzania wakati wa Picha ya Pamoja na Wenyeviti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Shk Kilemile pamoja na Rais wa Wanataaluma Waislam Bro. Mussa Mziya. Kutoka Kushoto ni Mussa Mziya (TAMPRO), Sheikh Arif (Islamic Foundation), Sheikh Mohamed Said (Independent Author), Sheikh Ramadhan Sanze (Baraza Kuu), Sheikh Suleiman Kilemile (Hay’at), Sheikh Jabir Katura (Msikiti Mkuu Mwanza) na Hajat Aisha Sururu (Aisha Sururu Foundation).
Mbunge CCM Al-Shaymaa Kwegyir akichangia ambapo aliitaka Jamii kumlea vizuri na kimaadili Mtoto wa Kike kwani mtoto wa kike akilelewa vyema ndio nguzo ya familia Kimaadili na wakati sahihi wa kumjenga kama nguzo ni kuanzia utotoni.
Katibu Mkuu wa Jumuia na Taasisi za Kiislam Sheikh Ramadhan Sanze akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari juu ya Changamoto na Maendeleo Mbali Mbali Jamii ya Kiislamu ya Tanzania hasa wanawake inayopiga wakati wa Kongamano.
Wanataaluma Wa Kiislam wakifuatilia kwa Makini Mada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan iliyowasilishwa na Sheikh Suleiman Amran Kilemile wakati wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan.
Wanataaluma Mbali mbali wa Kiislamu wakimsikiliza kwa makini Ustaadh Bakari Kombo Bakari kutoka Zanzibar alipokuwa akiongelea nafasi ya Muislam Mwanamke Wakati wa mtume Muhammad (SAW), Kabla yake na Mazingira ya Mwanamke leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2013

    tuhudumie wanaadamu wenzetu ndiyo kazi anayotakiwa kuifanya kila mwanaadamu, kila la kheri na Muumba awalipe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...