Mabondia wa bigright boxing ya mwananyamala wapo kambini wakiendelea kujifua kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao ambao watazichapa nao katika wakati tofauti na maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. 
 Mabondia hao ni issa omar anaetarajiwa kuzipiga katika ukumbi wa Government complex nchini zambia na Pethias Chisonga wa Zambia chini ya uratibu wa Exodus Stable ya nchini humo. Hapa Dar es salaam Friends Corner hotel Mustafa Doto atazipiga na Rajab Mjeshi, Martin Richard na Mbena Rajab wao watakuwa mkoani Tanga huku Zumba Kukwe akizipiga Kibaha na mabondia waliobaki watamsidikiza Daudi Anthony’Odinga’ kuzipiga na Tom-po katika ukumbi wa Eagles pub Bagamoyo. Katika mapambano ya Bagamoyo yameratibiwa na Tan academy chini ya kiongozi wake Japhet Kaseba yatakuwa na ushindani mkali sana kwa wanafunzi watano wa Kaseba watakapozipiga na wanafunzi wa Bigright nje ya mkoa wao
 Baadhi ya mabondia toka kambi ya Bigright boxing club wakiwa  kambini kwenye gym yao Mwananyamala jijini Dar es salaam wakijiandaa kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika siku ya idd.
 mabondia wa bigright boxing wakiwa mazoezini katika gym yao iliyoko mwananyamala
 Sparring ya nguvu
 Big right Ibrahim kamwe akiwa na vijana wake gym
 Tizi likiendelea
Vijana wakiwa tayari kwa mapambano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2013

    Hivi kwa nini mabondia wetu huwa wanfanya mazoezi kwenye mazingira duni na machafu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2013

    LAKINI WANASHINDA PAMBANO KAMA YULE ALIEMCHAPA MTHAILAND AMBAE ANAFANYA MAZOEZI KWENYE MAZINGIRA MASAFI NIA TU KUIPENDA KAZI YAKO AMA MCHEZO WAKO NA KUJITUMA KWA UJUMLA.
    ASANTE

    ReplyDelete
  3. ni kweli mabondia wa Tanzania wapo katika mazingira mabovu kutokana na mchezo wenyewe kutojaliwa na wenye uwezo hivyo mabondia wanajiendesha wenyewe kama yatima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...