Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kushoto) akishiriki swala ya Magharibi na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wa Mkoani Arusha, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza baadhi ya wananchi wa mkoani Arusha kuchukua futari, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiagana na wageni wao baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR.
Ankali plz muwe munacheki spellings kwanza jamanii. 'AFUTARU' au 'AFUTURU'? Hilo tu.. kazi nzur na blog nzur Tanzania nzima. Ramadhan Kareeem
ReplyDeleteHivi hii pesa ya kufuturisha kila mara wanavyofanya viongozi wa serikali ni pesa kutoka mifukoni mwao au kodi ya wananchi??
ReplyDeleteKama ni kodi ni nani amewapa mamlaka ya kutumia hizi kodi kwa mambo ambayo si ya serikali as serikal haina dini?
Michuzi tafadhali usiibanie hii comment hata kama wewe upo serikaln..this needs to be explained maana si sahihi kutumia kodi kwa mambo binafsi yenye kupendelea dini moja!..je wakristo, wapagani,ect wakiamua kufuturishwa kwa sikuu zao nchi itakwenda hii??
mdau
new york
Spot on mdau wa NY, I have had enough of these futaris kwa kutumia hela za wananchi. Tuelezeni wazi kama ni wao wanalipa au vipi?
ReplyDeleteSpot ON
ReplyDeletemdau new york hapo juu, udini tu ndio unaokusumbua,kwani watu wakikutana kwenye vikao hawanywi chai au lunch au diner???? kama ndivyo basi vp wakiamua kuahirisha hiyo lunch na ikaliwa jioni sababu wanakua wamefunga? mheshimiwa yuko kikazi,..wivu ni tu unakusumbua wewe!!
ReplyDeleteHivi mke wa mhe. JINA ASHA AU ZAKIA?
ReplyDeleteRukhsa nanyie kufuturishwa kwenye Kwarezma. Muhimu mfunge kweli tuu.
ReplyDeleteSijui ulishawahi kujiuliza pia pesa ya kupamba mapambo ya thamani kila aina kwenye ofisi za Serikali na kutuma zawadi za kadi na mivinyo kwenda kwa watu mbali mbali pesa hizo zinatoka wapi??
Jiulize kote kote na utafakari pia.
Serikali haina Dini ndio lakini watu wake wana Dini. Ni jukumu lake kuwatumika.
Jamani mimi ni muislam..lakini huyo mdau wa NY anapoint haijajibiwa kiutaratibu..swali lipo wazi..hajakataza kufurisha anachotaka kujua na mimi pia nahitaji kujua kuwa...viongozi hao wa serikali hizo futari wanalipia waumini na wanakaribisha viongozi kama wageni..au viongozi wenyewe wanatoa mifukoni mwao kama sadaka au serikali inalipa ili tujue bajeti ya kufurisha inatoka wapi...jamani tuwe wastaarabu tuhishimu dini za watu..
ReplyDeletemdau wa NY usishangae sana tz kila kitu kinakwenda kwa mazoea hata kama hayo mazoea ni kinyume cha sheria!
ReplyDeleteHushangai mtu anakamatwa na kosa then akiwa kituo cha polisi inapigwa simu kwa mkubwa na mkubwa anatoa amri aachiwe na anaachiwa maramoja!
wenyewe wanaita "utaratibu tuliojiwekea"!!
j4
ujerumani