Mume wa Marehemu Dkt Judith Kahama Maro, Profesa Maro, akiweka shada la maua juu ya kaburi wakati wa mazishi ya mkewe yaliyofanyika Alhamisi jioni katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. Marehemu, aliyekuwa mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alifariki dunia Julai 6, mwaka huu
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua juu ya kaburi la mama yao
Wazazi wa marehemu, Sir George Kahama na Mama Janeth Kahama wakiweka shada la maua kaburini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua
Mama Anna Mkapa akiweka shada la maua kaburini
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Said Meck Sadik, akitoa heshima zake baada ya kuweka shada la maua. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...