Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah akikabidhi kombe la ubingwa kwa timu ya Mbaspo kutoka Mbeya baada ya kufanikiwa kushindwa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya wahasimu wao Mbeya City katika faili ya kombe la Muungano Mufindi 2013 na kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya kushoto akiwa na mmoja kati ya wachezaji wa timu ya Mbaspo wakionyesha kombe la ubingwa leo katika uwanja wa shule ya Msingi Wambi mjini Mafinga.
Mabingwa wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi mwaka 2013 timu ya Mbaspo ya Mbeya katika picha ya pamoja na mashabiki wageni rasmi na wadhamini jioni ya leo katika uwanja wa Wambi mjini Mafinga.
Na Francis GodwinBlog
Timu ya Mbaspo kutoka mkoani Mbeya jana imeibuka bingwa wa mashindano ya kombe la Muungano 2013 baada ya kuigagadua kwa jumla ya mikwaju ya paneta 5-4 timu ya Mbeya City katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Wambi mjini Mafinga mchezo ulioshuhudiwa na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah.
Katika mchezo huo timu zote mbili ziliweza kuonyesha soka kali lililofanya mashabiki kujigawa katika kuzishangilia timu hizo ambazo zote mbili zilikuawa katika uwanja wa ugenini.
Mbali ya timu ya Mbeya City kujipatia mashabiki wengi kipindi cha kwanza wa kuishangilia ila hali iligeuka na mashabiki robo tatu ya uwanja kuamua kuelekeza ushabiki wao kwa timu ya Mbaspo kutokana na viungo wake nambali 4 na 14 mgongoni kuuteka uwanja huo kwa soka safi.
Hadi timu zote mbili zinakwenda mapumziko kipindi cha kwanza hakuna timu iliyobahatika kuchungulia lango la mwenzake .
Kasi ya mchezo ilionekana kubadilika kipindi cha pili kwa timu zote kukamiana bila mafanikio hadi mwamuzi wa mchezo huo alipopuliza filimbi ya mwisho kuhitimisha mchezo huo bila bingwa kupatikana .
Ili kuwa kazi ngumu katika upigaji mikwaju ya penati ambapo timu ya Mbeya City ilijikuta akipoteza nafasi moja na kutoa nafasi kwa timu ya Mbaspo ambao walijipanga vema na kufanikiwa kuingiza nyavuni mikwaju yote mitano na hivyo kufanikiwa kuibuka bingwa kwa kuingiza nyavuni mikwaju 5-4 na kufan ikiwa kutangazwa mabingwa katika michuano hiyo.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza timu ya Mbaspo imekabidhiwa pesa kiasi cha Tsh milioni 3 Mendani na kombe ,mshindi wa pili Mbeya City akinyakua mendani na Tsh milioni 1.5 wakati mwamuzi bora na mchezaji bora kila mmoja akinyakua Tsh 400,000
Mratibu wa mashindano hayo Daud Yassin Amewapongeza wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kampuni ASAS LTd ya Iringa,kampuni ya Mwananchi Communication,NSSF,Pareto, Ibrahim Khamis, PPF,MUcoba Benk na Chai Bora kwa kufanikisha mashindano hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...