Mahmoud Ahmad Arusha.

Meya wa jiji la Arusha Afyatuka awataka wanasiasa kuwapelekea wananchi maendeleo na kuachana na kauli za kumuondoa meya huyo na malumbano yasiyo na tija kwa wakazi wa jiji hili kwani utaratibu wa kanuni na sheria zipo wazi na hazihitaji malumbano  kwani yupo kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha Meya huyo Gaudency Lyimo alikuwa akijibu swali aliloulizwa kumekuwepo na malumbano ya muda mrefu kiasi cha kupachikwa majina kuwa meya wa kichina huku wanasiasa wakijinadi kuwa ataondoka kwenye kiti hicho baada ya uchaguzi mdogo uliopita mjadala wa meya hauna tija kwa wakazi wa jiji hili.

Meya Lyimo alisema kuwa wakati huu si wa kulumbana bali ni wakati wa kuwaletea wananchi maendeleo kwani siku hazirudi nyuma na wanaofikiri mawazo hayo wanakosea kwani kila nchi inasheria na kanuni walizojiwekea na hata halmshauri inaongozwa kwa mujibu wa sheria hivyo suala hilo lipo kisheria .

Lyimo Akawataka wanasiasa  wanaopita kuhoji uhalali wa meya huyo  kuwa ataondoka wanandoto za mchana kwani yeye yupo kisheria na kanuni zinazoendesha halmashauri hapa nchini huku akiwataka madiwani waliochaguliwa kuweka mbele maslahi ya wakazi wa jiji hili na kuwaletea maendeleo.

“Hapa suala si meya suala ni kuwaletea maendeleo wale waliokuchagua hapa utakuwa umetimiza majukumu yako kama diwani au mwanasiasa utakuta watu wanashindwa kuwatetea wananchi na kuanza kuilumbana hilo silo wananchi wanalihitaji bali wanahitaji maendeleo wao hawaangalii vyama bali watakudai maendeleo tu”alisema Meya.

Malumbano hayo yalianzishwa baada ya uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye jimbo la Arusha kwa chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA)kudai kuwa muda wa meya huyo unahesabika kwani idadi yao au koramu inatosha kumuondoa meya huyo.

Huku vyombo mbali mbali vya habari vikiripoti kuwa meya akalia kuti kavu ndipo waandishi walipoamua kumuhoji mmeya huyo kupata msimamo wake kwenye suala hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    mwandishi umenipa kazi kweli kusoma na kuelewa andiko lako. Najua kazi unaipenda, jitahidi basi usiache elimu.

    ReplyDelete
  2. ArchitectJuly 17, 2013

    yeye ameleta maendeleo gani kipindi chote hiki? ukiacha hata maendeleo ya jiji zima, ndani ya kata yake ya oloirieni, hakuna linalofanyika la maendeleo...kata haina soko,dispensari, wala huduma za zoa taka, barabara mbovu...wanakwangua leo kesho mashimo.ukienda kule utafikiri uko kijijini, kumbe ni mjini.watu wanajenga mpaka barabarani, na mtoni. yaani ni vurugu tupu utafikiri hakuna serikali.

    aanze kurekebisha kata yake ndo awashauri na wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...