Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari wa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni huki Darfur nchini Sudani wakati wakilinda amani,yakishushwa kwenye Ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,Jijini Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki duni Darfur wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia huko Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.
Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini leo majira ya alasili kwa kutumia ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.
Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.
So sad, may allah rest their soul in eternal peace, I personally argue Tanzanians to be pattient at this difficult time .
ReplyDeleteRespect to all soldiers in the country!
Natoa pole kwa famila za marehemu.
ReplyDeleteMungu apunzishe Roho zao mahali pema peponi.
Amen
R.I.P mashujaa wetu
ReplyDeleteWakati umefika wanajeshi wetu tusipeleke bila ya kuwa na silaha za kujihami. Huwezi kulinda amani bila ya mlinzi mwenyewe kuwa na silaha ya kujihami.
ReplyDeleteRIP you all,inauma sana jamani!
ReplyDeleteSerikali imesema kila familia inapata fidia ya shs milioni 113, fedha hizo ziwafikie wajane kwa ajili ya watoto na sio kwa mashemeji au mawifi tafadhali!
Hakika tutawakumbuka daima mashujaa wetu,poleni sana wafiwa,tupo nanyi ktk wakati huu mgumu
ReplyDeleteTuhakikishe msiba huu hauna mko wa maadui wetu.(M23 na Kagame)Kama kuna mkono wa Kagame then TUMSHIKISHE ADABU kama tulivyo fanya kwa NDULI wa Uganda.When it came to milirary "We are the supper power in East Africa".
ReplyDeletePOLE kwa WAFIWA wote
MUNGU IBARIKI TANZANIA.