Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya China Power Investment ambaye jina lake alikupatikana.
 Balozi wa China hapa nchini Mhe. Lu Youging akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia,kulia ni Rais wa Kampuni ya China Power Investment,  Lu Qizhou

 Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akiweka saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia, waliosimama kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youging na  Rais wa Kampuni ya China Power Investment,  Lu Qizhou
Baadhi ya wajumbe kutoka Kampuni ya China Power Investment wakifuatilia zoezi la uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia. 
Picha Zote na Frank Shija, MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2013

    kila siku ukiangalia picha za wawekezaji utaona wana miili ya kawaida yenye umakini wa kujilinda na maradhi

    na ukiangalia wanaowekezewa au wazalendo utawaona wamevimba mavitambi mashavu yani wana shape za kuendekeza njaa na ufisadi fisadi wa umma na ndio maana miili yao imevimbiana hovyo kwa kulakula bila mpangilio

    watanzania tujiweke miili yetu kimpangilio wa kupambana na magonjwa sio kujiachi tu na kukaribisha magonjwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2013

    Bongo ukiwa na fedha lazima uvimbe, maana hukuzipata kwa kufanya kazi, umechota somewhere. Waliomiss ndiyo wembamba kama mimi. Check out!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2013

    wamesoma vizuri mkataba lakini??? isijekua kama mambo ya IPTL, songosongo sijui kina nani wale ambao waliamua kuzima mitambo eti kukarabati mabomba ya gas wakati kulikua na line nyingine ambayo ingetumika.....nina shaka sana na hawa wawekezeka, ila lets wait and see

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2013

    Nakubaliana asilimia mia moja kuhusu life style yetu hasa ulaji,wengi tunadhani kuvimba ni afya. Nadhani ankal ututafutie mtu mfano kaka Macha atoe somo la chakula, wengi tunapokuwa na hela tunajitia kuingia supermarket kununua vyakula vya makopo,hapo ndio tunajiua,. Inabidi tuelimishwe mapema, angalia Marekani na jirani Afrika kusini watu wanavyoteseka na uzito

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2013

    aliyevimba mashavu hapo ni nani? mbona macho yangu yanaona mashavu ya mchina na mswahili sawa tu labda tofauti ni ni namna yalivyo kaa hata wachina wenyewe wametofautiana,..nani mnene hapo? mbona prof. na huyo DG wa tanesco ni wakawaida tu? haya maradhi ya kuangaliana kwa jicho baya na kudhaniana nia mbaya tu yatakwisha lini? ni lini tutajua lipi zuri na baya wanalofanya watanzania? nadhani tunatakiwa kutoka nje ya box..na ikiwezekana nje ya nchi nyengine labda siku moja tutapata uzalendo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2013

    hawa wanaendeleza yale yale ya IPTL, Dowans, na Symbion. ni bora kuwapa mkopo tanesco au tpdc wanunue hiyo mitambo ya kuzalisha umeme.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2013

    Umeme wenyewe mpaka sasa shida mnatuletea habari ya kuuza.. Siasa bwana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...