IMG_8897  
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (katikati) akipata maelezo ya kazi mbalimbali za Shirika hilo kutoka kwa Afisa Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8935
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (katikati) akimuonyesha Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (kulia) malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo hicho ambapo mafunzo hayo yanadhaminiwa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
IMG_8946
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na wanafunzi wa Chuo cha DIT kwenye banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
IMG_9000
Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Wanafunzi wa Chuo cha DIT cha Mwanza.
IMG_8976
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akizungumza na waandishi habari ambapo amefafanua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia katika mabadiliko ya tabianchi ambapo wao kama Umoja wa Mataifa wanafanya kazi ya kuelemisha Umma, Wakulima, Wafanyabiashara na Wasindikaji jinsi ya kuelelewa mabadiliko ya tabianchi katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa njaa duniani na upatikanaji wa chakula. Kulia ni Mratibu wa kazi za vijana vijijini katika masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa FAO Bw.Eliamoni Lyatuu.
IMG_8968
Afisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akitoa ufafanuzi wa vipeperushi mbalimbali vinavyozungumzia kazi zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini kwa baadhi ya vijana na watoto waliotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
IMG_8980
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakifurahia picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2013

    VIONGOZI WA TANZANIA KAMA WANGEKUWA WASIKIVU, WANGESIKIA HILI.

    Katika kila miji mikubwa wangebuni "Maduka maalum" ama pengine Mitaa maaluma wangeipa jina mfano " made in Tanzania bussiness Centre" kwa lengo la kuuza na kuwezesha urahisi wa bidhaa za Tanzania, tofauti na ilivyo sasa msimu kama wa saba saba kuna bidhaa nyingi, nzuri na imara za kitanzania ajabu baada ya maonesho utazipata wapi?

    Kimsingi wenye mamlaka lazima bongo zichemke tofauti na ilivyo sasa tuna mezwa na bidhaa toka nje.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2013

    Nakubaliana na anonymous hapo juu. Nadha bidhaa zatengenezwa kwa ajili ya maonyesho tu! Baada ya maonyesho hawatengenzi tena. Lakini kwenye ripoti pesa zinaonekana zimetumika kununua mali ghafi. Ukisema unaitwa mkorofi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...