Kongamano la siku 3 kujadili dawa bandia limefunguliwa leo na naibu waziri wa afya, Mheshimiwa Dr. Seifu Rashid. Kongamano hili linahudhuruwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali Africa zikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Botswana, South Africa, Zambia, Eritrea, Ethiopia, Madagascar, Zimbabwa, Namibia na Mozambique. Pia kuna wawakilishi toka USA na makao makuu ya shirika la afya dunia (WHO).

Wajumbe wa kongamano watapata nafasi ya kujifunza mfumo mpya wa kompyuta wa jinsi ya kutoa na kupata taarifa mbalimbali juu ya dawa bandia.

Kongamano linafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), uliopo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mr Hiiti B. Sillo, Mkurugenzi wa TFDA akitoa utangulizi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Naibu waziri, Dr. Seifu Rashid akifungua rasmi kongamano hio, kulia kwake ni Michael Deats, kutoka makao makuu Shirika la Afya Duniani (WHO)
Sehemu ya washiriki wa kongamano.
Nchi za Africa zinazowakilishwa kwenye kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2013

    katika mtiririko wa herufi, mbona naona kama R inamiss au imelazimika kuiondoa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2013

    Nyuma ya Tanzania naona Zanzibar je nayo ni nchi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2013

    Nimejaribu kuitafuta hiyo nchi inayoitwa ERYTHREA katika google na ramani zote, bado sijaiona. Wadau naomba mnijuze, nchi hii ipo bara gani na basic facts zake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2013

    ERYTHREA labda ni moja ya dawa bandia kama zile za ARV bandia za Tanzania na kesi yake hatujui imeishia vipi kama ilivyo jina la nchi ERITREA lilivyopotezwa hapa jijini DSM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...