Habari na Picha Na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii Moshi.
WIZARA ya maji,imeelezea kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa kampuni
ya usambazaji maji wilayani Rombo ya Kiliwater kwamba haijajipanga
kibiashara na ingeweza kupata faida kubwa kuliko hali waliyonayo sasa
kama wangekuwa makini.
Naibu waziri wa maji Dk Binillith Mahenge alitoa kauli hiyo baada ya
kupokea taarifa ya kampuni hiyo kuhusu usambazaji wa huduma za maji na
mipango yao katika ununuzi wa mita kwa ajili ya kuwafungia wateja wao.
“Kwa mipango hii mliyonayo kama kampuni hii ingekuwa imekabidhiwa
mfanyabiashara yeyote makini,angeshindwa kupata faida?” alihoji huku
mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Silayo akikiri kwamba faida
ingepatikana.
Aliitaka kampuni hiyo kujipanga upya kwani wanayo fursa ya kupata
faida kama wakijitahidi kupunguza maji yanayopotea lakini pia
kuhakikisha wanaondokana na mfumo wa ulipaji anka kwa ‘Flat rate’ bali
wawafungie wateja mita za maji.
“Huu mfumo wenu wa watu wote kulipa maji kwa viwango sawa unawapotezea
mapato, wapo wanaoyatumia kwa ajili kumwagilia migomba kasha watalipa
sh 3,000 kwa mwezi, ninyi mnaona hilo ni sahihi,badilikeni”alisema.
Katika baarifa yake kwa naibu waziri meneja wa Kiliwater, Prosper
Kessy alisema uzalishaji wanakabiliwa na uzalishaji mdogo wa maji
usiokidhi mahitaji kwani upo upungufu wa mita za ujazo 13,000 sawa na
lita 13,000,000 kwa siku.
Alisema pia wanakabiliwa nupungufu wa mita za ujazo 22,000 sawa na
litaza ujazo 22,000,000 wakati wa kiangazi na hivyo kuongeza tatizo la
maji kwa wateja wake.
“Kiwango kikubwa cha asilimia 78 ya maji yasiyouzwa kutokana na
uchakavu wa miundombinu,wazi wa maji,wateja wasio na mita na wale
wenye mita lakini hutumia maji kiholela”alisema.
Hata hivyo alisema kampuni hiyo inahitaji zaidi y ash milioni 600 kwa
ajili ya kuwafungia mita wateja wake kama njia moja wapo ya kuongeza
mapato
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akikagua miradi ya maji katika wilaya ya Rombo.
Mhandisi wa maji wilaya ya Rombo Andrew Tesha akitoa maelezo kwa naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge alipotembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo.
Naibu waziri wa maji Dk Mahenge akikagua mradi wa maji wa kilichopoeneo la hifadhi yam lima Kilimanjaro(KINAPA)
Naibu waziri Dk Mahenge akizungumza na mhandisi wa maji wilaya ya Rombo Andrew Tesha alipotembelea kisima cha maji katika kijiji cha Ushiri.
hivi we waziri unawafikiria wananchi au unafikiria faida tuu swala la msingi wananchi wapate maji. Kwa hiyo bill inayolipwa 3,000 kwa mwezi sehemu ndogo ilobaki serikali ongeza sio we unataka kuongezewa mshahara tuu bila kufikiria wananchi hasa vijijni ambao wengi hawana kazi wanategemea hicho kishamba alichoachiwa na babu yake apate nusu ya debe kahawa, auze na haina bei ndio matumiz ya mwaka mzima. Jamani hebu kuweni na imani na wananchi so faida tuuuuu
ReplyDeleteWaulize hao KILIWATER wanataka wananchi wachimbe mitaro ya maji kwa nguvu zao, watandike mabomba ya maji alafu wao waje wakusanye pesa kwa kuwawekea mita. Kwa nini msichimbe mitaro kwa gharama zenu na kufunga mabomba ya kisasa ili maji yasipotee bure. Mnategemea mabomba yaliyofungwa na mkoloni kupata faida?
ReplyDelete